Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemfungia kiungo wa Yanga Pius Buswita mwaka mmoja kwa kosa la kusaini kwa wakati mmoja mikataba na timu mbili tofauti yaani Simba na Yanga akitokea Mbao FC.
Hayo yameweka wazi baada ya kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoongozwa na Wakili Richard Sinamtwa, ambayo ilikutana Agosti 20 mwaka huu Jijini Dar es Salaam kupitia usajili wa majina ya klabu 40 uliyofanywa katika kipindi cha usajili.
Kamati hiyo ilibaini kwamba mchezaji huyo aliyechezea Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita Pius, amevunja Kanuni ya 66 ya usajili Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaelekeza adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha jina la Kidao Wilfred kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo.
Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ameteuliwa rasmi jana Agosti 22, 2017 na Kamati ya Utendaji ya TFF