Sumatra, Tanroads na Polisi Waikana Faini ya Sh 200,000 ya Mwendokasi...Watoa Ufafanuzi Huu


Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazozua mkanganyiko kwenye mitandao ya kijamii kuhusu faini zinazotoshwa na Wakala wa Usimamizi wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa madereva wanaozidisha mwendo wa magari au kufanya makosa mengine ya barabarani.

Kufuatia mkanganyiko huo, Balozi wa Usalama Barabarani (RSA) ambao hujitolea kutoa elimu ya usalama barabarani kuhakikisha watumiaji wote wa barabara wanakuwa salama.

Katika ufafanuzi huo uliotolewa na RSA, kwanza walianza kujibu swali ambalo liliulizwa na wengi kama TANROADS ina mamlaka ya kupiga faini kwa kosa la mwendokasi.

TANROADS kama mamlaka ya usimamizi wa barabara chini ya Sheria ya Barabara (ROADS ACT 2007) inayo mamlaka ya kuwaadhibu wale wote wanaokiuka mwendo uliooneshwa kwenye alama za barabarani au kadiri ya maelekezo yao.

Mamlaka haya wanayapata kwa mujibu wa kifungu cha 32(2) cha Sheria ya Barabara, Na.13 ya mwaka 2007. Hata hivyo, ili mtu atozwe faini chini ya sheria hiyo ni hadi atiwe hatiani.

Inayotia mtu hatiani ni mahakama, hivyo ukikamatwa na TANROADS unatakiwa kufikishwa mahakamani na huko ukipatikana na hatia uweze kutozwa kiasi cha shilingi 200,000 au jela mwaka 1, na sio vinginevyo.

Jambo jingine lilitotolewa ufafanuzi baada ya kuzua maswali ni kama kweli faini za barabarani zinazotozwa kwa kosa la mwendokasi sasa ni sh 200,000 na inagawanyika mara tatu yaani kiasi cha shilingi 90,000 kinaenda SUMATRA, Shilingi 30,000 kinaenda Polisi na inayobaki ni ya TANROADS.

RSA wameeleza kwamba, madai hayo ni upotoshaji. Faini ya chini ya sheria ya barabara ni shilingi 200,000 kwa kuzidisha mwendo kinyume na kifungu cha 32(2) na haigawanyiki.

“Haiwezekani kutozwa faini zaidi ya moja kwa kosa hilo hilo. Kwani sheria inasema mtu hataadhibiwa mara mbili kwa kosa hilo hilo alilolitenda mara moja. Iwapo mtu ameadhibiwa mara mbili adhabu hiyo ya pili ni batili. Ndio kusema kwamba, hata mamlaka zote 3 ziwepo pamoja, ukikamatwa umezidisha mwendo utaadhibiwa mara moja tu na mamlaka ile iliyokukamata.”

Mabalozi hao walilazimika kulielezea hilo baada ya kuwepo swali kama inawezekana mtu mmoja akaadhibiwa na mamlaka zote tatu kwa pamoja endapo zitakuwa barabarani kwa wakati mmoja eneo moja zinafanya operesheni.

Kuhusu uwepo wa sheria 3 kwa jambo hilo hilo moja la kuzidisha mwendo, imeelezwa kwamba kila sheria ilitungwa kipindi tofauti na nyingine na kila sheria inasimamiwa na mamlaka yake bila mamlaka moja kuiingilia nyingine.

SUMATRA anasimamia Transport licensing Act Cap 317 na kanuni zake, ambapo faini ni kati ya shilingi 200,000 na 500,000. TANROADS inasimamia Roads Act 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009, ambapo faini ni shilingi 200,000 huku Polisi wakisimamia Sheria ya Usalama Barabarani (Road Traffic Act Cap 168) ambapo faini yake ya papo kwa papo ni shilingi 30,000 bila kujali ukubwa au udogo wa kosa.

Kila mamlaka inasimamia sheria yake na kwamba mamlaka moja mfano Polisi hawawezi kukuandika faini kwa kutumia sheria ya TANROADS. Kama watataka kufanya hivyo watalazimika kukukabidhi kwa mamlaka hiyo.

Washirikishe na wenzako waweze kupata elimu ya usalama barabarani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad