Tanzania Kujengwa Maabara ya kisasa ya Afrika

Tanzania Kujengwa Maabara ya kisasa ya Afrika
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya Teknolojia ya Nyuklia kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki nchini (TAEC) Arusha, maaabara ambayo inatarajiwa kuwa ya kisasa kwa vifaa Afrika.

Akizungumza na viongozi mbali mbali wa mkoa huo na watumishi wa taasisi hiyo, Waziri Ndalichako amesema maabara hiyo ni ya watanzania na hivyo watumishi wanaofanya kazi katika tume hiyo  wasifanye kazi kwa ubinafsi na badala yake watangulize maslahi ya Taifa mbele.

Majengo ya maabara hiyo ya kisasa yanatarajiwa kukamilika Februari Mwaka 2018 ambapo yatagharimu kiasi cha shilingi   Bilioni 2.3, na ikikamilika Umoja wa Ulaya itafunga vifaa vyenye thamani ya Sh. Bilioni 11 ambapo  tayari baadhi ya vifaa vya Sh. Bilioni 2.6 vimekwishawasili nchini.

Pia Waziri na viongozi wengine wa Wizara wametembela Chuo cha Veta sehemu ya kuzalishia umeme kikuletwa pamoja na Chuo cha Ualimu Elimu Maalumu Patandi, kwa lengo la kukagua miundombinu ya chuo hicho pamoja kujionea vifaa vya kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Viongozi wengine ambao waliambatana na waziri kwenye ziara hiyo ni pamoja na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Mhandisi Stella Manyanya na Naibu Katibu Mkuu, Profesa Saimon Msanjila
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. YES YES YES...!!! hapa ninakueleweni katika dhana ya Tanzania ya Viwamda na uchumi wa kati. HAPO TUTAONDOKANA NA SHIDA YA UMEME KWA MIAKA MIA TATU IJAYO NA VIWANDA INAWEZEKANA. NA TUNAWEZA KUWEKA NATIONAL GRID NA TUKAWAUZIA JIRANI WEMA...MAMA NDALICHAKO ITS A RIGHT DECISION ON THE RIGHT DIRECTION...BABA MAGU WATAKUELEWA TU NIA NA LENGO LAKO KWA TANZANIA YETU NI WENYE AKILI NDIO WATAKAO KUFAHAMU KWA HARAKA. MUNGU AKUBARIKINI KWA NIA NJEMA ZENU JUU YETU NA VIZAZI VYETU. HISTORIA ITASHUHUDIA HAYA..HAKUNA KUREMBA. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad