Trump Aapa Kushinda Vita Afghanistan

Trump Aapa Kushinda Vita Afghanistan
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutaacha pengo ambalo huenda likajazwa na magaidi.

Alisema kuwa mapango yake ilikuwa ni ya kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambao yalitokea nchini Iraq.
Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.

Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi
Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.

Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.

Rais Trump ameitupia lawama Pakistan kwa madai kuwa inawahifadhi magaidi ambapo amesema suala hilo linapaswa kuachwa mara moja.
Katika hatua nyingine amezungumzia mpango wa Marekani kuimarisha mpango wa ushirikiano na India.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad