Uingereza Yaitaka China Kuzungumza na Korea Kaskazini

Uingereza Yaitaka China Kuzungumza na Korea Kaskazini
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa Uingereza itaimarisha juhudi zake kukabiliana na ukatili wa Korea Kaskazini wa kufanyia majaribio makombora yake , lakini akaitaka China kuimarisha ushawishi wake dhidi Pyongyang.
Akizungumza wakati alipokuwa akielekea nchini Japan kwa ziara, alilaumu Korea Kaskazini kwa vitendo vya uchokozi.

Ziara hiyo ya waziri mkuu pia inalenga kupigia debe biashara mbali na kuwahakikishia washirika wake kwamba hatua ya Uingereza kujiondoa katika muungano wa Ulaya haitaathiri chochote.Bi May amesisitiza kuwa majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini ni kinyume na sheria.
Alisema:Tutaongeza juhudi zetu na washirika wetu wa kimataifa kuishinikiza Korea Kaskazini kusitisha vitendo hivyo vinavyokiuka sheria.

Amesema kuwa Uingereza imeshirikishwa katika mazungumzo ya kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini mbali na kutafuta mabadiliko ambayo China inaweza kufanya.
Amesema kuwa China ina jukumu kubwa huku akiitaka Beijing kufanya kila iwezalo kuishinikiza Korea Kaskazini.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe alitaja jaribio hilo la kombora la Kaskazani kama tishio lisilo la kawaida kwa taifa lake huku baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likiishutumu Korea Kaskazini kwa pamoja.

Wakikutana usiku wa Jumanne mjini New York, baraza hilo lilitaja urushaji wa kombora hilo kama wa kikatili huku likitaka Korea Kaskazini kusitisha jaribio lolote la makombora yake.
Lakini Korea Kaskazini imetoa ishara ya kurusha makombora zaidi ,ikisema kuwa hatua yake ya kurusha kombora kupitia anga ya Japan ni mojwapo ya mipango yake ya kijeshi katika eneo la Pacific.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad