By Fred Mpendazoe
Shujaa wa Tanzania Hachaguliwi kwenye Makongamano yanayofanyika nje ya nchi yetu. Hao ni Mashujaa Wao.
Katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti yameandika kuhusu baadhi ya wanachama wa chama kimoja cha siasa hapa nchini kukamatwa na polisi na kuwekwa mahabusi na baadae kuhojiwa na kupelekwa mahakamani. Wanachama hawa wamekamatwa kwa tuhuma mbalimbal zikiwemo kufanya uchochezi au kukaidi maelekezo waliyopewa na vyombo vya usalama. Wengine wamekamatwa kwa kutumia lugha chafu kwa viongozi hasa wa chama kinachotawala ambao wamepata ridhaa ya watanzania wengi kuongoza nchi. Kama makongamano yanayofanyika nje ya Nchi yetu wanawaona watu hawa ni mashujaa, ni mashujaa wao siyo mashujaa wa Nchi yetu.
Serikali ya JPM ndiyo iliyochaguliwa na watanzania wengi na iko kikatiba, hivyo ni halali. Hivyo serikali ya JPM siyo ya dikteta.Kumekuwepo madai kwamba JPM anawanyanyasa watanzania na hashauriki. Siyo kweli, JPM analo baraza la mawaziri linalomshauri na anacho chama chake kinachomshauri. Pia anao watalaam wanaomshauri katika masuala mbalimabali.Hivyo hola hizi hazina mashiko.
Kwa muda mfupi, serikaliya JPM imeonyesha mwelekeo wenye kuleta matumaini kwa mwatanzania.
- JPM ameonyesha dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi ukilinganisha na baadhi ya vyama vinavyompigia kelele kwamba ni dikteta.
- JPM anapiga vita rushwa, uzembe kwenye serikali, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
- JPM anachukua hatua kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watanzania wengi
- JPM anasimamia kwa karibu watendaji na kufuatilia kwa karibu kero za wanachi, hakuna ombwe la uongozi.
- JPM ameweza kuchukua maamuzi magumu, mfano elimu bure; mchanga wa madini usipelekwe nje ya nchi.
- Hatua alizochukua JPM dhidi ya wizi bandarini na sehemu nyingine zinaonyesha uzalendo wake.
- JPM anatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi ya chama chake kilichopewa ridhaa kuongonza na watanzania.
Kwa hatua hizo alizochukua JPM ni mtanzania yupi mzalendo ambaye amenyanyaswa au kuonewa kwa hatua hizo ? Au kwa hatua hizi mtanzania yupi anagandamizwa ?
Kwa ujumla, JPM ameleta heshima kwa nchi yetu hadi nchi za nje zinaanza kuchukua hatua ambazo JPM amezichukua hapa Tanzania.
Mtanzania yoyote anayenung’unika kwa hatua hizi zilizochukuliwa na serikali ya JPM ni dhahiri uzalendo wake una walakini na nidhahiri pia anapigania maslahi yake binafsi au ya kukudi cha watu fulani wachache wala si maslahi mapana ya nchi yetu.
Lakini pamoja na hayo yote baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani tena wenye elimu nzuri wana mkejeli na kumwita JPM eti dikteta uchwara, KWELI INASIKITISHA.
Lakini, ni kwa lipi hasa wamwite dikteta uchwara?
Wapo wanachama wa chama kimoja wanawasifu hawa viongozi waliokamatwa na kuachiwa kwa dhamana eti ni mashujaa.
Je ni kipi cha maana na heshima kwa nchi yetu wanachokipigania hadi waitwe mashujaa?
Ushujaa wao ukowapi? Je kukamatwa na kuwe kwa rumande kwa kuitukana serikali ni ushujaa ?
Je kuwekwa rumande na baadae kupata dhamana kwa kuandamana bila kibali cha polisi ni ushujaa ?
Je kukamatwa na vyombo vya dola kwa kukaidi maelekezo ya vyombo hivyo ni ushujaa?Hapana. Kama kwenye mikutano au makongamano yanayofanyika nje ya Nchi wanawaita mashujaa ni mashujaa wao siyo mashujaa wetu.
Wanachokifanya wanachama hawa ni upotoshaji wenye lengo la kuvuruga amani ya Nchi yetu. Watanzania tukatae upotoshaji huu na tuwapuuze. Nawasihi watanzania tuiunge mkono serikaliya JPM.
Juzi kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Demokrati huko Marekani Mama Obama amewatahadharisha na kuwataka wamarekani kuwapuuza viongozi wanaotukana ovyo hadharani kwani wanajenga fikra mbaya kwa vijana wa Marekani. Mama Obama alikuwa anamzungumzia mgombea wa chama cha republican ambaye nimsema ovyo, ambaye ana lugha ya matusi kwa viongozi na amekuwa akimtukana rais Obama kwenye mikutano.
Mama Obama ameuliza, Je vijana wa Marekani wanajifunza nini kwa viongozi hawa wanaotumia lugha chafu hadharani? Ni dhahiri maadili ya vijana wa Marekani yatakuwa hatarini. Kwa mtazamo huo wa Mama Obama, vijana wetu hapa Tanzania wanajifunza nini wanaposikia lugha za matusi kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa ?.
Vita ni siasa inayomwaga damu kwani haina majadiliano wala ushawishi. Ni ugomvi.Vyama vya siasa viepukane na ugomvi. Vijenge hoja na viwashiwishi watanzania kuhusu sera zake.
Je ikitokea kijana akamwambia baba yake kwamba ni baba uchwara atajisikiaje?Au akakuambia wewe mama ni mama uchwara. Je utafurahi jirani yako akimpongeza huyo kijana na kumwita shujaa ?
Je haiwezekani kudai haki na demokrasia na kutoa maoni na kuikosoa serkali bila kutumia matusi na kejeli kwa serikali iliyoko madarakani?.Upinzani ujifunze kwamba, siasa za kiuanaharakati kwa Tanzania hazikubaliki. Tanzania iliisha pata Uhuru wake.
Tukumbuke Nyerere alidai uhuru kwa kutumia hoja za msingi hadi wakoloni wakatoa uhuru. Siasa ni vita isiyo mwaga damu. Ni majadiliano na ushawishi. Hata sasa inawezekana kudai haki, kutoa maoni na kuikosoa serikali bila kutumia lugha ya matusi.
Mtu yeyote asiyetaka kuongozwa hawezi kupata fursa ya kuogoza.
By Fred Mpendazoe
Toa Maoni Yako
Uanfishi wako wa shida. Kuona kwako na mtazamo wako nishida pia. Waandishi chukueni kazi yenu seriously. Na muandikapo zameni ndani zaifi kabla hamjaana
ReplyDeleteZa. Si kila mwandishi anabidi w
Awe mwandishi.wstu hawasemi haya ypte jinsi ulivyoandika. Kuna nia njema sana na Magufuli.na ameamua kusahihidha yale maraisi wstatu wa ccm waliomtangulia wameyasababisha hii wate kwanza tukubaliane.
Je kama yeye ni kiongozi wa ccm mbona hajatamka kwamba jamani kilio chenu nimekisikia na ninayasafisha yale wenzangu walionitangulia waliyasababisha.
2 haya yalisababishwa kwani katiba yetu dhaifu, ili kuhakikidha haya mambo hayarudii tena, nitasaini hii katiba mpya ya Wariobs ili kuhakikidha kila atakayekuja na kudhindwa kutekeleza majukumu yake itakuwa rahisi kumchukulia hatua.
3.ingekuwa ni rahisi kwa nchi kwake kutumbua madudu yote kwa kufuata sheria za nchi bila kumwachia yeyote hata akiwa raisi kwani maraidi waliopita ndio vinara waliosababisha haya yote anayoyasahihisha.
Kinachotokea sasa, anachagua jinsi anavyoona yeye, nani atumbuliwe na nani asitumbuliwe.na hii inaleta shida kisheria. .ulimuona alivyomsifia Kafulila vizuri, je yule sliyemwita tumbili si ndiye slikuwa jaji mkuu hakutoa hukimu nyingi na hakudimamia sheria, chini yake hawa wahujumu wengi wsliachiwa huru, mbona hajachukuliwa hatua. Hawa wote ni viongozi wakuu wa serikali ambao walichaguliwa na kupewa dhamana ya nchi na wengine kuteuliwa.ni hawa inambidi asitie visingizio vyovyote na kutokuwagusa, na hii inawasumbua wengi, hawa nfio madingi wskuu nchini waliilainsha sheria kwa miaka nenda rudi kuruhusu nvi iende mrsma na magavana wa benki. Hawa nfio wsliobariki akina rugemslila na wenzake wachukue pesa za umma. Hwa nfio wslidimamia na kuikubslia mikatsba yote hii wanashetia na marsidi wa nchi hii na wskuu wa mabenki na mawaziri wa ccm wakishirikuana na wabunge wengi wa ccm.Naye pia alikuwa ni mmoja wso. Unajua ni vigumu kuona kibanzi chsko jichoni.Hawa wakubwa wanaolindwa bado wspo kwenye maofisi na wengine ndio wanaomsapoti je unafikiri watamsapoti kuwstumbua wenyewe. Na bado wanatenda kazi na kujisifu. Kazi za kimaendeleo sababu wanamifuko ya pesa hii haileti picha nzuri. Ukiwsona maraisi wengine wa nchi nyingine wamemaliza muda wso hawapoo kila siku madarakani kama maeaisi wa Tanzania.mpaka tuone anawatoa wale wahusika wakuu wote hapa nitampa mkono asilimia mia moja.Ingawa najua anajitahidi kwa namna fulani lakini atafanikisha zaidi akiwa strong zaifi kukata kiini cha matatizo hayo ambayo wote tungemuunga mkono, kusaini katiba ambayo ingrlinda mali za watanzania badala ya kuleta visheria vichache kwa dharula bungeni, kstiba ingerekebidha haya yote na mengine. Nyinyi waandidhi shida hamjazamia ndani zaidi kikazi, na hoja zenu haziendi ndani na kuchimbua ukweli uliopo. Mnapaka mafuta mambo na kuacha mambo mazito njr.wala hamuendi mbali kudadisi ni nini kimetuleta hapa tulipo. Na uandishi kama huu hauelimushi umma na ni upotoshaji pia. Nendeni mkapate mafunzo bora ya uandishi ambao utaelimisha watu na si wa namna hii.
hivi wewe anonymous wa 14:17 mbona unatuvurugia kiswahili chetu???kama kuandika hujui acha nenda kacheze chandimu maana mara nyingi unachangia ushuzi tu.
DeleteAnonymous3 August 2017 at 14:17 - uanonesha kuchanganya mada!Aliyoyasema Mpendazoe ndiyo ukweli wenyewe ingawa kwako ni shubiri. Tunataka kiongozi anayechukua hatua katika kutatua matatizo ya wananchi. Hizo bla bla huu siyo wakati wake. Kitaeleweka tu!
ReplyDeletesawa kabisa mpendazoe. umezungumza na umefikisha ujumbe baada ya uchambuzi ni sahihi.. huyo anonimasi wa14 ndio qale wale wa kule kuvuka Reli madongo polonoka wamejaa uji kwenye nyewele..Hapa kazi tu.
ReplyDelete