Ukweli Mchungu...Kinachoendelea Nchini ni Ubaya Kwa Ubaya...Hatuna Budi Kujirekebisha Kabla Mambo Hayajaaribika


Bila shaka wote tunafahamu ni nani ametufikisha hapa! Jamii zinafanyiana ubaya ubaya. Ubaya unalipwa kwa ubaya!

Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala inayiendekea juu ya matukio ya kisiasa na kijamii yanayiendelea nchi hii. Kwa ufupi naweza kusema nchi imepoteza kabisa mshikamano.

Tumekuwa kama familia maadui na mahasimu kiasi kwamba kila familia inaiombea nyingine majanga au ishindwe katika jambo fulani.

Tumefikaje katika hatua hiyo?
Wapinzani na wafuasi wao wamejengewa chuki na serikali iliyopo madarakani. Serikali iliyopo madarakani imewafanyia wawakilishi wao ubaya.......imewabeza, imewafunga, imewadharirisha, imewatukana na kuwanyima haki zao za kikatiba! Wapinzani wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao,kila wanachosema kinabezwa!

Lakini kubwa zaidi na linalouma ni kudhalilishwa na kufanyiwa ukandamizaji wa hali ya juu. Hili limeleta chuki kubwa sana.

Hata sharia ya makosa ya mitandao utekelezaji wake umekuwa wa kibaguzi. Wanaokamatwa ni wale Wanaoukashifu upande fulani. Lakini Lowasa, Mbowe, Lissu, Maalimu Seif wanakashifiwa na kutukanwa sana. Hapo ndipo wafuasi wa niliowataja hapo juu wanaona kumbe sheria zinatungwa kibaguzi kama wakati wa makaburu South Afrika.

Mfuasi wa Tundu Lissu hawezi kuwa tayari kuiunga mkono serikali wakati unamtesa na kumdhalilisha mwakilishi wake. Mfuasi wa Bulaya na Heche anaona uonevu anaofanyiwa mbunge wake,hivyo amejengewa chuki ya hali ya juu sana. Serikali ikishindwa kwake ni furaha.

Serikali ielewe kwamba hivi ndivyo namna magaidi wanavyozaliwa, Boko Haram na Alshabaab ndivyo ilivyoanza, jamii moja kuona inaonewa na nyingine.

Maana yake ni kwamba Serikali imekuwa ikilazimisha mshikamano wakati matendo yake ni kinyume.

Wakati upinzani ukiomba intelijensia za nje kama CIA isaidie kumtafuta Ben Saanane serikali inasema hapana,hapo unategemea wafuasi wa Ben, wafuasi wa upinzani na ndugu wa Ben wanaitafasiri vipi serikali?

Dola ionekane ikitenda haki badala ya kusema tu wananchi waiunge mkono serikali! Binafsi naona kuna mambo serikali inafanya poa, lakini ninapooana wapinzani wananyanyaswa namna hii, najikuta sioni cha kuipongeza serikali, yoote yanakuwa yamemezwa kwenye uonevu

Imeandikwa na  Boban Sunzu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukweli uchungu kinachoendelea nchini kwa upande wa Chadema ni kupigania ukanda ukabila nakadhalika. Tanzania kuna serikali moja tu na kama taasisi nyengine yeyote inajaribu kujifanya serikali lazima serikali halali itumie vyombo vyake vya dola kuchukua sheria. Wapinzani na wafuasi wao hasa Chadema wanaendesha siasa katika misingi ya chuki, Hofu kwa wananchi, uzushi na baya zaidi kuendesha kampeni za makusudi kuipiga vita serikali iliopo madarakani ishindwe kutekeleza mipango yake ya kuwaletea wananchi maendeleo. Tumemuona Lisu na washirika wake walivyolifuraikia suala la ndege ya Bomberdier kuzuia. Tumemuona Lisu na washirika wake walivyopambana vya kutosha kuhakikisha suala la Makinikia lisitafutiwe ufumbuzi ili wazungu hao waendelee kuibia Tanzania. Tulimuona Lisu na washirika wake wanavyopambana kuhakikisha Tanzania inanyimwa misaada ya maendeleo na jumuia za kimataifa,Tumemuona Lisu na washirika wake wanavyohamasisha watanzania kutotii utawala wa sheria. Kwa hivyo kama ubaya kwa ubaya sasa hizo kelele za kulalama kuwa mnaonewa ni za nini? Mmeamua kuipiga vita serikali halali ilioko madarakani mlitegemea nini kutoka kwa serikali?
    Chadema ndoto zenu za mchana za kufikiri siasa zenu za kiuwanaharakati mnaikomoa serikali ni kujipotezea muda na mwisho wa siku mtaumia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad