Ummy Mwalimu Aagiza Wahudumu wa Afya Kutoa Huduma Bora kwa Wajawazito

Ummy Mwalimu Aagiza Wahudumu wa Afya Kutoa Huduma Bora kwa Wajawazito
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili.

“Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji,” alisema Waziri Ummy.

“Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.

Hata hivyo alisisitiza kuwa wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine vinavyoweza kusababisha uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad