Msanii Grace Matata ambaye kwa sasa yupo nchini ya usimamizi wa kampuni kubwa ya kimataifa ya kusimamia muziki, ya Pana Music, ametoa maelezo kuhusu aina ya muziki anaoufanya na kusababisha mashabiki wengi kutomuelewa na kumkubali.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Grace Matata amesema muziki wake ni wa tofauti lakini una 'impact' kubwa, kwani yeye anafanya muziki unaoishi muda mrefu.
"Lengo langu ni kufanya muziki ambao unaishi kama Angelique Kidjo, ukimuangalia Angelique Kidjo muziki anaoufanya watu wengi hawaujui, lakini umemfanya achukue mpaka tuzo ya Grammy, huo ndio muziki ambao nafanya, muziki wangu hauitaji kiki ili niwe maarufu, watu wengi hawauelewi muziki wangu lakini watu wanaojua muziki mzuri wanauelewa sana ndio maana nafanikiwa kufanya show za live kila wiki na yenye kiingilio kikubwa", alisema Grace Matata.
Pia Grace Matata ambaye jana amezindua wimbo wake mpya wa 'Dakika Moja' akimshirikisha Wakazi, amesema yeye lengo lake ni kwenda kimataifa zaidi na ndio maana hata lugha anachanganya, ili hata watu wa nje waweze kuelewa muziki wake.
Keep it up Grace, napenda sana Mziki wako ni mkomavu.
ReplyDelete