Upelelezi wa Polisi Nyumbani kwa Tundu Lisu Wamaliza

Upelelezi wa Polisi Nyumbani kwa Tundu Lisu Wamaliza
Jeshi la Polisi limemaliza  upekuzi waliokuwa wanafanya nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu  Lissu  wanaelekea  Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam.

Taarifa ya msemaji wa Chadema Tumaini Makene amesema Lissu anapelekwa polisi  kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria kuendelea  ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo kisheria iko wazi.

Amesema upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo  ya kumkashifu  rais na  Uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi Huyu Makene kaajiriwa na Nani? na Wadhifa gani?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad