Ushauri Alioutoa Ney wa Mitego Kwa Ali Kiba, Dimpoz Pamoja na Diamond

Ushauri Alioutoa  Ney wa Mitego Kwa Ali Kiba, Dimpoz Pamoja na Diamond
Wakati vita baridi ikiendelea kuunguruma huko mitandaoni kati ya wanamuziki Diamond, Ally Kiba na Ommy Dimpoz, rapa Nay wa Mitego ameibuka na kutoa neno lake la kukemea kuwahusisha wazazi katika mabifu yao.


Licha ya Nay kuwahi kuimba kwenye ngoma yake mstari unaosema, “nampenda demu wangu kuliko mama yangu”, lakini ameonekana kuguswa na kuchukizwa na kitendo cha Dimpoz, kumhusisha mama wa Diamond katika ugomvi wao.

“Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.
nay wa mitego

“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,” aliandika Nay wa Mitego katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad