Video: Makonda Awatoa Hofu Wakazi wa Dar Sakata la Bomoa Bomoa

Makonda Awatoa Hofu Wakazi wa Dar Sakata la Bomoa Bomoa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo August 30, 2017 ametembelea eneo la bomoabomoa Toangoma katika Wilaya ya Temeke na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ishu ya bomoabomoa katika eneo hilo.

Akiwa katika eneo hilo RC Makonda amewatoa wasiwasi wananchi ambao wamekuwa na hofu baada ya kuambiwa watabomolewa nyumba zao lakini akawaambia kuwa hakuna atakayewabomolea nyumba zao.

”Nawaomba tujiepushe na sehemu hatarishi, kila kinachofanywa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaokoa wananchi. Hakuna mtu atakayewabomolea nyumba zenu, hata Rais aliniambia hamkumchagua ili awabomolee nyumba zenu.

“Tulikubaliana na Rais kuwa nyinyi mjiepushe kujenga kiholela na kwenye maeneo hatarishi na mfuate utaratibu.” – RC Makonda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad