Kwanza wanatakiwa kutambua kuo mziku huo ni harakati ambao unalenga hasa kuelimisha jamii na kuonyesha uhalisia wa maisha na katika utendaji wa viongozi wetu
Bahati mbaya wasanii wetu ambao wanajaribu kuimba nyimbo za harakati wameanza kwenda kinyume na malengo hayo kwa kuanza kuelezea hisia zao za makundi
Katika huo wimbo wa juu wasanii hao wawili wamejisifia zaidi ktk kuwakubali baadhi ya watu wakasahau kuwa wao kama wanaharakati sio watu wa kusifia au kuwa upande fulani...wao wanatakiwa wawe kwa wale watu ambao wanaenda sawa ndio wanaweza kuwasifia lkn sio kuwa kubali
Mwanaharakati unatakiwa usifie lakini sio kuwa kubali watu maana kumkubali mtu yaani ww hata akikosea ni sawa tu
Lakini pia wao wanatakiwa kujua wana carrier kubwa sana katika industry na zaidi mashabiki zao wamegawanyika
Hivyo basi nawashauri wanaharakati wa mziki wasiweke wazi msimamo wao kwamba wana mkubali mtu fulani bali ikiwezekana wamsifie tu inatosha kuepuka kuleta mgawanyiko ambao unaweza kuleta chuki
Kwa wasanii kama hao kuimba nyimbo zenye kuleta matabaka ni uchochezi wa wazi...maana wanajaribu kuleta chuki baana ya pande mbili
Napenda kuwasihi sana wasanii wetu wawe waangarifu sana huku wakizingatia maslahi ya taifa kama watu wamoja