Vita vya Wahenga....Master Jay Apingana na Mzee Kitime Katika Hili....

Producer mkongwe wa muziki wa bongo Fleva Master Jay, amesema anapingana na kauli iliyotolewa na mkongwe mwenzake kwenye tasnia ya muziki mzee John Kitime, aliposema kwamba hakuna mtu anayeweza kutikisa tasnia ya muziki kwa kazi yake yoyote ile.

Akizungumza na mwandishi wetu Master Jay amesema anatofautiana na Mzee Kitime kuhusu hilo kwani wapo watu ambao walifanya vizuri kwenye muziki na kuandika historia, akimtolea mfano msanii Ferouz kwa wimbo wake wa starehe, ambapo uliweza kumpatia mafanikio makubwa sana.
"Kwa haraka haraka sikubaliani naye, sijui anatumia vigezo gani anaposema hivyo, unajua watu wa enzi hizo mara nyingi wanaangalia vipaji, sasa hivi watu wengi hawana vipaji ila ni wafanya biashara wazuri, kwa mfano kipindi kile hao hao kina Ferouz kwa wimbo mmoja huohuo ulimpa mafanikio makubwa, alinunua Jeep kipindi ambacho hata kununua pikipiki ni ngumu, ndio maana nasema sikubaliani", alisema Master Jay.

Lakini Master Jay aliendelea kusema kuwa kama anaangalia kwa wasanii ambao wanafanya muziki sasa hatokuwa na kipingamizi naye, kwani sasa hivi wasanii wengi wanafanya muziki wa biashara na sio kipaji kama ilivyokuwa zamani, hata kwa nje ya Tanzania.

"Sasa hivi watu wanafanya muziki kwa computer, hata nje wanafanya muziki kwa computer, ukiwa na kipaji siku hizi ukiimba sana watakwambia kaimbe kanisani, hata hawa wanaojifanya 'concious rappers' hawafanyi vizuri, ila kama anamaanisha hivyo ni sawa", alisema Master Jay.

Master Jay ni producer mkongwe kwenye muziki wa bongo fleva, ambaye unaweza  ni mmoja wa waasisi wa muziki huu ambaye alishawahi kutengeneza nyimbo zilizotikisa tasnia ya bongo fleva.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad