Zikiwa zimebaki siku mbili watani wa jadi Simba na Yanga kukutana katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara 2017/18 alimaarufu kama Ngao ya Jamii, klabu ya Yanga yatangaza wachezaji wake ambao hawataweza kucheza mchezo huo.
Klabu ya Yanga ambayo inatarajiwa kuingia nchini siku ya Jumanne ya tarehe 22 Agosti mwaka huu ikitokea visiwani Pemba Zanzibar ilipoweka kambi ya wiki nzima kujiandaa dhidi ya Simba imesema wachezaji wake watatu akiwepo Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa , Benno Kakolanya na Mwasiuya kutokana na kuwa majeruhi.
Aidha klabu hiyo imesema kuwa imejipanga tayari kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya wapinzani wake wa jadi na kusema hali kikosini iko salama wanasubiri mchezo husika ambao utapigwa siku ya Jumatano tarehe 23 Agosti uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mitandao ya jamii bado tambo mbalimbali zimekuwa zikiendelea dhidi ya watani hao wajadi huku kila upande ukijigamba kuwa katika mchezo huo wao wataibuka na ushindi wa hali ya juu, huku wengine wakidai kuwa huenda Simba inaweza kurudi historia yake ya kuifunga Yanga kwa goli