Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa ni mwanasiasa mpinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali, atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.
Akiwajibu wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.
“Sitaki na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria mpaka ndoto zao zilipotimia.
“Kagame alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa, Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka 36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.
Hivi karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.
sasa wewe zito unajifananisha na hao maraisi yaani unatamaa kuwa siku moja uyakuja pata cheo nchi hii yetu. eewe ea kalemii. mbona unaota mchana. kwanza unahadhi hiyo unavyo jutathmini? wacha hizo polojo zako na kuota mchana. Dogo.
ReplyDeleteKutaka kuwa rais sio tamaa bali ni utashi walikuwa wanasiasa karibuni wote duniani. Zitto Ana yo hadhi ya kuwa rais isipokuwa wewe unachuki binafsi ambazo unatakiwa uombe mungu akusaidie uachane na chuki, zitto ni mtanzania wa kuzaliwa na nimsomi
DeleteIkiwa makonda anaweza kuwa mkuu wa mkoa mkubwa na tajili tanzania basi zitto anaweza kuwa sio tu rais bali mfa
me
jAMANI HUYU NI KIJANA WANGU.. LAKINI INAVYOELEKEA NA JINSI ANAVYO JIFANANISHA NI DHAHIRI KWAMBA WAYA ZINAANZA KUGONGA MIAMBA. NA KULE KWAO PIA WANAMUELEWA HIVYO. UKITAKA KUJUA MUULIZE KAFULLLA.
DeleteMPAKA MFALUME ALISHA PATA KUWA KABLA YA SIKU CHACHE. NA ALIVYO AMKA AKAJIKUTA KALALA KWENYE GALI.
ZILE MADA ZA KUNYAPIA ZIMEKWISHA MTAANI WITH FULL RIGHT OF OWNERSHIP TO JPM.
KWA HIYO UPUMZIKE VILIVYO MPAKA NILIVYO KWAMBIA KESHO NA KUTWA.
HAPA NI KAZI NA KAZI KWELI KWELI. UPUUZI HATUTAKI NA MAKONDA NI MMOJAWAPO NNAMKUBALI KWA UCHAPA KAZI WAKE.
Hivyo huoni Haya ... Wewe wa kuleeeeeeee. AhHHhhhh SIKUELEWI. Hivyo unajielewa mwenyewe?
ReplyDelete