Klabu ya Simba kesho Jumamosi itaendelea na Semina elekezi kwa wanachama wa wilaya za Ubungo, Kinondoni , na Ilala , zenye lengo la kuwajengea uelewa mpana zaid juu ya muundo mpya wa klabu, uliotokana na mabadiliko makubwa ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao.
Semina hiyo ya tarehe 19-8-2017, itaanza saa sita mchana kwenye jengo la Ngawaiya liliopo Manzese Argentina upande wa kushoto kama unaelekea Ubungo,katika Barabara kuu ya Morogoro.
Pia Siku ya Jumapili hii ya tarehe 20-8-2017,kuanzia Saa mbili asubuhi, klabu itafanya Mkutano mkuu maalum wenye lengo hilo,ili taratibu za kuingia kwenye muundo mpya zianze kufanya kazi.
Mkutano huu muhimu na wa kihistoria, utafanyika pale pale tulipofanyia Mkutano mkuu wa kawaida wiki iliopita, Mwalimu Nyerere International Conference Centre uliopo maeneo ya Ocean road hapa jijini Dar es salaam.
Tunawaomba wanasimba kokote walipo waje kuweka historia hii muhimu,historia itakayofanywa muandikwe kwa wino wa dhahabu, Historia ya kuitoa klabu ilipo na kuipeleka mbele zaid, kiuchumi, kibiashara, kimafanikio ya uwanjani, na pia kuwa klabu ya kwanza nchini kuingia katika muundo huu,unaokusudia kuifanya Simba iwe moja ya klabu bora kabisa Afrika.
Mwisho
Niwaambie maandalizi ya Mkutano wa Jumapili ni kabambe na kila kitu kimekaa sawa, pengine kuliko Mkutano wa wiki iliopita.