Wanaume Watakiwa Kupima Tezi Dume





Wanaume Watakiwa Kupima Tezi Dume
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ma Watoto, Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wanaume kupima saratani ya tezi dume huku akiwatoa hofu kuwa kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume unapima kwa kutoa damu na sio kipimo kinachotembea mitandaoni.



Waziri Ummy ametoa wito huo mkoani Katavi Manispaa ya Mpanda pamoja na wananchi waliotoka wilaya ya Mlele na Tanganyika mara baada ya kuzindua zoezi la upimaji magonjwa ya sio ya kuambukizwa.

“Lakini inaweza kuwa wanaume mnaogopa kupima saratani ya tezi dume na mimi nitoe wito kwa wanaume mpime kwasababu pia sio kile kipimo kinachotembea mitandaoni kipo kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume ambapo unapima kwa kutoa damu na sio vile mnavyofikiria kile kipimo ambacho watu wanakiogopa hicho sicho kipo kipimo rafiki,” aliongeza Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya wasiotoa huduma za kuridhisha na wenye kashfa ya kutokuwa na maadili ya kazi.

“Pale ambapo muuguzi amekujibi vibaya, daktari amekujibu vibaya na mkunga hajakufanyia vizuri, wauguzi wa hospitali ya Mpanda wengi ni wazuri tutajie jina na sisi tutamchukulia hatua na tutamwambia atupishe wapo watu wengi sana wanaotaka kufanya kazi katika hospitali za serikali,” alisema Ummy.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad