Wapiga Debe Waiomba Serikali Kusitisha Mpango wa Kuwaondoa



Wapiga Debe Waiomba Serikali Kusitisha Mpango wa Kuwaondoa
Zaidi ya vijana 200 ambayo wanaopiga debe eneo la Kamanga Ferry jijini Mwanza, wameiangukia serikali na kuiomba iwaache waendelee na shughuli zao na kusitisha mpango wake wa kutaka kuwaondoa hapo, anaandika Moses Mseti.

Vijana hao wametoa kilio chao kwa Katibu wa Umoja na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Mwanza, Mariam Amiri.

Mwenyekiti wa wapiga debe hao, Husein Manyika, amesema baada ya kusikia tangazo la serikali kupitia vyombo vya habari ambalo linawataka kuondoka na kuacha kazi hiyo, limewashtua na kwamba hawajui pa kwenda.

Amesema kuwa katika eneo hilo pia wapo wapiga debe, wachuuzi wa samaki pamoja na wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga.

“Tunaambiwa tuondoke hapa (Kamanga), wakati serikali haijatuandalia maeneo ya kutupeleka hivyo kabla hawajatuondoa, wanapaswa kukaa na watafakari ni wapi watakapotupeleka ndipo wachukue uamuzi huo,” amesema Manyika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad