Wasanii wa Bongo Nani Kawaroga? Kila Msanii Anataka Kwenda Kimataifa Kumbe ndo Mnajiaribia...

Wote wamekalilishwa neno "kimataifa" utacheka sana namna wanavyokazania huu ujinga... Madee katoa nyimbo mpya kamshirikisha Tekno wa Nigeria alooo nyimbo ni mbaya dunia nzima, shishi kamshirikisha mdada wa Nigeria asee nyimbo ukiidownload unaifuta saa hio hio baada ya kumaliza kuiskiliza, yote tisa joh makini ndio kachekesha sanaa, katoa nyimbo na davido ni mbaya ukiiskiliza mpaka unaweza kuumwa kichwa, nyimbo nzima unaskia tu kataa kataa leetaa hawa nani kawaroga?

Mbaya zaidi wanatumia mamilioni kuwalipa wasanii hao wanaowaita wa kimataifa na utengenezaji wa videos ambazo hakuna anaejisumbua ata kuziomba kwenye TV stations.

Tulitegemea labda wasanii wetu hawa watakua wajanja na wabunifu kidogo labda, ila wao wameimba kama wanaija tu hali inayopelekea kupoteza muda na fedha.

Kujua ni kujua tu, hakuna aja ya kupoteza muda kwa watu ambao ata nao hawajatoboa kimataifa kama uyo sijui IYO nk., sasa hawa wanao jiupgrade na kujiita wa kimataifa ila wanategemea show moja ya fiesta maishani wanajiskiaje wakiona mtoto mdogo kama Aslay tu ambae video Zake uenda ni za elf 50 tu ila uswahilin kote nchini zinapigwa kama nyimbo za taifa na youtube ngoma zake zinatoboa views million Mpaka 2+, lazima watajidharau tu ila na kwa vile wasanii hawa ni mbumbumbu Hawawezi kureason hapo.

Sasa unakuta msanii chege alishafanya nyimbo mpaka na run town ila sasa nna uhakika hata malawi hawajui kama kuna mbumbumbu anaitwa chege, huyu simlaumu kwakua amekua akilazimisha fani, ila sana wale wenzake daaah hasa joh maskini huyu yeye tulijua anatoboa maana davido huyu huyu kabisa? Davido kaishika africa kwa sasa unapata bahati adhimu alaf unaimbaa kataa kataa leta wewe umerogwa au? Hio hela ya mavideo ya gharama ya nyimbo mbaya kama hio si bora uyo msanii angeenda kununulia ng'ombe tu zikaja kumsaidia maishani.

Anyway, wasanii wetu bado hawajajua kua wanapoteza muda na fedha kutafuta vitu wasivyovijua, big up diamond wasaidie ndugu zako.

Mjumbe wa kihenga hauwawi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad