Washukiwa wa Mauaji ya Mkurugenzi TEHAMA Kenya Wakamatwa Uganda.....
0
August 06, 2017
WASHUKIWA WA MAUAJI YA MKURUGENZI TEHAMA KENYA WAKAMATWA
Jeshi la Polisi nchini Uganda linawashikiliwa watuhumiwa 3 (Mkenya 1 na Waganda 2) wa mauaji ya Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, Chris Msando.
Msando alitoweka nchini Kenya na kupatikana akiwa amefariki. Polisi wa Uganda wamesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na gari aina ya Toyota Fortuner. Gari hilo lenye namba za usajiri za Uganda huku ikidaiwa lilikuwa na namba za Kenya wakati wa kuvuka mpaka wa Busia.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi majira ya saa 9 alfajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
Marekani na Uingereza zilikubali kutoa maofisa wao wawili wa ngazi za juu kutoka mashirika ya upelelezi ya FBI na Scotland Yard baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Keriako Tobiko kutaka uchunguzi ufanywe kuhusu mauaji ya Msando. Aliitaka pia serikali kuhakikisha usalama wa maofisa wa IEBC ili uchaguzi ufanyike kwa usalama.
Polisi walisema mwili wa Msando uligunduliwa katika msitu wa Kikuyu na kumbukumbu za mochwari zinaonyesha kwamba ulipelekwa hapo Jumapili asubuhi pamoja na mwili wa mwanamke mmoja asiyefahamika uliopatikana sehemu hiyohiyo.
Jeneza lenye mwili wa Chris Msando.
Marehemu Msando ameelezewa na marafiki zake kuwa mwalidifu na mcheshi, ambapo wafanyakazi wenzake katika IEBC wakiwemo Andrew Limo, Tabitha Mutemi na Ronnel Onchagwa wakisema alikuwa na utaalam mkubwa wa teknolojia, mwadilifu na mcheshi. Kabla ya kupatikana kwake, gari lake lilikutwa likiwa halina mtu eneo la Roysambu, Nairobi.
Source: Daily Nation
Tags