Kitengo hicho kilimnukuu afisa Dungu Christophe Ikando akisema walijitambulisha kuwa wale wa LRA.
''Tunashutumu utekaji wa watu 10 kutoka kijiji cha Kunu na watu waliojihami kwa bunduki ambao walijitambulisha kuwa waasi wa LRA''
Idhaa ya redio ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa takriban watu 40 walitekwa ikiwemo maafisa wawili wa tume ya uchaguzi nchini humo.
Ettiene Akangiambe ambaye ni afisa mkuu wa tume hiyo ya CENI alitibitisha habari hizo.
''Maajenti wetu wawili ambao walikuwa wakirudi kutoka katika kituo cha kusajili wapiga kura walivamiwa na watu hao waliojihami''.
Waasi wa LRA wanekuwa wakifanya operesheni zao nchini Uganda, DR Congo na Jamhuri ya Afrika ya kati CAR na Sudan kwa miongo kadhaa lakini uwepo wao umepungua kufuatia operesheni za kieneo na zila za majeshi ya kimataifa.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba LRA limewaua takriban watu 100,000 na kuwateka watoto 60,000 tangu lianzishwe na Joseph Kony 1987.
Mnamo mwezi Mei , wanajeshi wa Uganda na wenzao wa Marekani walitangaza kwamba wanasitisha operesheni yao ya kumsaka Kony ambaye alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita 2005 na uhalifu dhidi ya binaadamu na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague.
Wasiwasi wa kisiasa umekuwa ukiongezeka DR Congo huku shinikizo za kumtaka rais Kabila kuandaa uchaguzi mkuu zikiendelea.
Muda wake wa kutawala ulikamilika mwezi Disemba mwaka uliopita na makubaliano ya kuandaa uchaguzi mwengine mwishoni mwa 2017 yaliafikiwa.