Hivi karibuni, toto wa Rais Mstaafu wa Marekani, Malia Obama alipoteza simu yake aina ya iPhone, na juhudi zake za kutaka kuibadili zilikumbana na kikwazo, tofauti na alivyotarajia.
“Malia alikuja kwenye duka la vifaa vya Apple ili aweze kununua iPhone nyingine na kurudisha taarifa za simu yake iliyopotea lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia,” alisema shuhuda aliyekuwa kwenye duka hilo jijini Chicago akiliambia jarida la New York Post. “Wahusika wa duka hilo la vifaa vya Apple hawakuweza kumtatulia shida yake haraka kwakuwa Malia hakuwa na namba yake ya utambulisho ya Apple (Apple ID) wala neno la siri la simu aliyopoteza kwakuwa vitu hivyo vilifanywa na maafisa wa Ikulu ya Marekani wakati baba yake akiwa Rais wa nchi hiyo.”
Malia Obama alikuwa jijini Chicago kuhudhuria tamasha la muziki la Lollapalooza.
Watumiaji wengi wa simu aina ya iPhone wanaweza wakawa wanajua kero hii inayotokana na kusahau namba zao za utambulisho za vifaa vya Apple na namba zao za siri zinazowawezesha kujisajili kwenye mfumo wa vifaa vya kielektroniki vinavyotengenezwa na kampuni hiyo.
Kero hiyo huongezeka baada ya kuingiza neno la siri lisilo sahihi kwa mara kadhaa jambo linalosababisha mtumiaji wa kifaa hicho afungiwe na kushindwa tena kutumia kifaa chake mpaka atakapopata msaada wa wataalamu wa kampuni hiyo waweze kumfungulia.
Kisha, unapoambiwa uandike namba mpya ya utambulisho — kama utakumbuka ile ya zamani! — Apple itakataa namba yoyote ambayo ulishaitumia awali na kukuhitaji uandike nyingine, jambo litalokuongezea uwezekano wa kuisahau katika kipindi kisichozidi wiki moja tu – na mzunguko huu unaanza upya utapopoteza simu yako.
Katika hali kama hii, kampuni ya Apple kusisitiza ulinzi wa wateja wake linaonekana kuwa na manufaa kwa watumiaji wa vifaa hivyo kwakuwa simu ya Malia bila shaka ina baadhi ya mambo ambayo ni ya siri ya familia yake na kutomfanya Rais Mstaafu wa Marekani apigiwe simu na tapeli au yeyote aliyehudhuria tamasha hilo na kumsababishia usumbufu