Waziri Mwijage Aogopa Kutumbuliwa Alia na TRA

Waziri Mwijage Aogopa Kutumbuliwa Alia na TRA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutomfukuzisha kazi kwa uzembe wao uliopelekea nchi kupigwa na kupata hasara kutokana na watu kuingiza cement kutoka nje ya nchi wakidai ni krinka.

Waziri Mwijaga alisema hayo jana kupitia kipindi cha HOTMIX na ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi.

"Mtu anatengeneza Krinka anauza Kenya, sasa kama mtu anatengeneza Krinka Tanga anauza Kenya wewe unafuata nini Pakistan? Hakuna krinka inatoka nje ya nchi ile ni Cement iliyokamilika TRA wanashindwa kufanya kazi yao, narudia kusema hakuna krinka inaingia nchini kutoka nje ile ni Cement kamili na anayepinga aje aniambie mimi, na kuanzia leo TBS wasikague krinka yoyote kutoka nje ya nchi waingize ndani ya nchi bila TBS kukagua, TBS ipo chini yangu sasa kama mimi naambiwa sitoshi na wa TBS ajiangalie" alisema Mwijage

Aidha Waziri Mwijage alidai kuwa watu wa Cement walikubaliana na DR Meru kununua hizo Krinka hapa hapa nchini
"Watu wa Cement walikubaliana hapa na Dr. Meru Twiga Cement ananunua Krinka Simba Cement mwingine nani ananunua krinka nyingine kutoka wapi, watu wanaleta cement iliyokamilika wanasema Krinka sasa kuanzia leo TBS hawezi kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi, mpaka mamlaka iliyopo juu yangu sasa kama TRA walizembea tukapigwa juu yao kwanini wanataka kuharibiana kazi, eti bwana wanataka kuniharibia kazi mimi" alisisitiza Waziri Mwijage




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad