Waziri Nchemba Atembelea Shule Mbalimbali na Kukuta Ubovu wa Miundombinu


Waziri Nchemba Atembelea Shule Mbalimbali na Kukuta Ubovu wa Miundombinu
Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara yake kutembela kila Kijiji katika kila Kata zilizopo Jimboni mwake kuzungumza na wapiga kura na kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Leo ametembela Kijiji cha Ujungu katika Kata ya Mekente na kukuta ubovu wa miundombinu katika Shule ya Msingi Ujungu katika kijiji hicho huku Walimu wakiishi katika mazingira magumu ambapo aliamua kulibeba jukumu la kuboresha miundombinu akiahidi kulishughulikia mapema iwezekanavyo.

Waziri Nchemba amesema “Kwa kazi nzuri mnayoifanya naahidi leoleo kwa kushirikiana na marafiki zangu tutatengeneza mkaakti wa kushughulikia ukarabati wa madarasa pamoja na nyumba za walimu, walimu tisa kukaa kwenye nyumba tatu hesabu hii haina uwiano kabisa”

“Hii ni hatua moja kubwa sana na baada ya miaka 15,20 utaona Mbunge anatoka huku, kwasababu hata kijijini nilipotoka walikuwa wanapaita kijijini hivihivi kwa hiyo nitakarabati darasa kama njia ya kuweka mfano bora” –Waziri Nchemba


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad