Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Amshukuru Kardinali Pengo

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Amshukuru Kardinali Pengo
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema  msaada wa uchimbaji wa kisima cha huduma ya maji safi na salama kilichochimbwa kwenye Kituo cha Mahabusu ya Watoto Upanga, kimeipunguzia Serikali gharama ya Sh4,800,000 zilizokuwa zinatolewa kila mwaka.

Kutokana na hatua hiyo Waziri Mwalimu amemshukuru , Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa kuhamasisha vikundi vya uinjilishaji na umisionari kuguswa na kujitolea kugharamia uchimbaji wa kisima hicho.

"Msaada huu ni mkubwa kwetu tulikuwa tunalazimika kutumia shilingi 400,000 kwa mwezi kwa ajili ya maji, ambazo sasa tunaweza kuzihamishia kwenye gharama za matibabu kwa kuwakatia bima ya afya watoto,anasema.

Kadinali Pengo kwa upande wake amesema katika misaada yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa jamii wanaepuka kuitoa kwa ubaguzi wa aina yoyote.

"Tunaweza kufanya hayo japo yanaweza kuonekana ni madogo lakini sisi tunasukumwa na upendo, hivyo tukifika mahali hatuulizi wewe ni dini gani au dhehebu gani tunapenda amani na upendo udumu kwenye jamii,"alisema.

Chanzo cha kuchimbwa kisima hicho ni kutokana na ziara waliyoifanya watoto wa Shirika la Utoto Kurasini kituoni hapo na kubaini changamoto inayowakabili watoto wenzao, hivyo wakaguswa na kuomba ushirikiano na vikundi  vingine vilivyowezesha kujengwa kwa gharama ya Sh 11,780,000

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad