Wema Amsaka Mtu wa Kutoka Naye Siku ya Uzinduzi wa Filamu Yake.

Wema Amsaka Mtu wa Kutoka Naye Siku ya Uzinduzi wa Filamu Yake.
Msanii wa filamu wa kike bongo Wema Sepetu ambaye wengi humtaja kuwa msanii mwenye nyota ya kupendwa na mashabiki, amefunguka kuwa anasaka mtu atakayetoka naye usiku wa uzinduzi wa filamu yake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amendika ujumbe wa kumtafuta mtu huyo atakayekuwa naye usiku huo, kwani akisema raha ya tukio kama hilo lazima uwe na mtu pembeni yako, kwani anatarajia kuvunja kabati kwa kupendeza, lakini haitakuwa na maana kama atakuwa peke yake.

" Bado siku 4 tu, nilisema kuna tatizo, kupendeza nitapendeza tena sana tu ila sasa sina date wa kwenda naye raha ya zulia jekundu uwe na mtu... nani atajitolea kuwa mtu wangu kwa usiku huo wa kukumbukwa!?", aliandika Wema Sepetu.

Mwisho wa wiki hii Wema Sepetu anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayotwa 'Road to heaven' aliigiza na wasanii wengie wakali wa filamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad