Wizara ya Elimu Yakanusha Uvumi wa Kupata Degree Bila Kupita Kidato cha 6

Wizara ya Elimu Yakanusha Uvumi wa  Kupata Degree Bila Kupita Kidato cha 6
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia imeutaarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa kwa kasi kwenye kichwa cha habari kuwa ” Serikali yapiga marufuku kusoma degree bila kupita kidato cha sita” sio za kweli na hazijatolewa na waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.

Wizara kupitia wizara yake imeutaarifu umma kuwa taarifa hizo ni taarifa za uongo ziliwahi kusambazwa pia kipindi cha udahili cha mwaka 2016.

Wizara hiyo imeendelea kusisitiza na kuufahamisha umma kuwa Waziri ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako hajatangaza chochote na popote na kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad