Wolper: Nipo Tayari Kwenda Jela Mtu Atakaye Maneno Machafu kwa Mzazi

Wolper:  Nipo Tayari Kwenda Jela Mtu Atakaye Maneno Machafu kwa Mzazi
Msanii wa filamu za bongo ambaye kwa sasa ni mjasiriamali mkubwa, Jackline Wolper, amekula kiapo cha kwenda jela iwapo mtu yeyote atamtolea maneno machafu mzazi wake.

Msanii wa filamu Jackline Wolper
Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Wolper amesema yeye kwa kawaida ni mpole lakini iwapo mtu atafanya kitu kibaya juu ya familia yake, hatofikiria mara mbili kumfanya kitu ambacho kitamsababishia kupelekwa jela.
“Kwa mimi binafsi Jackline Wolper ni mpole, lakini ukija kwenye issue za wazazi mi nitaenda Segerea, ndiyo maana hujawahi kusikia Jackline Wolper kamuweka mama yake au baba yake kwenye instagram, kwenye Tv, yani sitaki wazazi wangu wahusike, nitukane mimi usitukane damu yangu, au usitukane mtu aliyenileta duniani, yani dakika sifuri nitapelekwa tu jela”, alisema Jackline Wolper.
Kumekuwa na tabia ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoleana maneno machafu mpaka kuwajumlisha na wazazi wa watu hao, kitu ambacho si kizuri kwenye jamii, kwani ni udhalilishaji wa watu wasio na hatia hususan wazazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad