Zito Kabwe Ashtushwa na Tukio La Bomu Ofisi ya Mawakili

Zito Kabwe Ashtushwa na Tukio La Bomu Ofisi ya Mawakili
Nimeshtushwa na tukio la bomu kwenye ofisi ya Mawakili wa IMMMA Advocates. Wakati tunaendelea kupata Taarifa zaidi nawasihi wanasheria wa kampuni hiyo kuwa na moyo wa subra na ninawapa pole Sana.

Kuna haja ya uchunguzi Huru kuhusu matukio ya aina Hii kwani yanamwelekeo fulani. Tukio kama hili lilitokea Kwa Wakili Omar Said Shaaban ambaye alikuwa anamtetea Ndugu Mansour Yusuf Himid. Sasa aina hiyo hiyo ya uhalifu imefanywa dhidi ya ofisi anayofanya kazi Wakili Fatma Karume ambaye ni mpwa wa Mansour. Tusiache mambo haya kuzoeleka hata kidogo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad