ZITTO Kabwe Aichana Serikali....."Watu Lazima Wahoji Swala la Ndege Mtake Msitake, Msilete Viroja Vyenu"

Mbunge wa jimbo la Kigoma Ujiji Mh. Zitto Kabwe amekingia kifua kauli inayotolewa na serikali ikiwashutumu vyama vya upinzani kushiriki na kutoa taarifa za ndege kuzuiliwa nchini Uingereza, na kusema kuwa kama wananchi wana kila haki ya kuhoji.

Akijibizana na baadhi ya wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter, Zitto Kabwe ameandika akisema suala kama hilo ni lazima watu wahoji, na sio kama hawapendi maendeleo yanayofanywa na uongozi wa Rais Magufuli, isipokuwa wanataka serikali ifanye vitu kwa uhakika zaidi, ili kuepusha kujiingiza kwenye hasara na migogoro kama hiyo.

“Watu ni lazima wahoji mtake mistake, hakuna anayetaka msubiri, tunataka mfanye Kwa  uhakika, tutaendelea kuhoji na lazima  serikali ijibu”, aliandika Zitto Kabwe.

Mh. Zitto Kabwe aliendelea kuandika “hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo, lakini ndege tunataka na tunapanda, mkihojiwa mnaleta viroja, jibuni hoja tu viroja vya nini ?”, aliandika Zitto Kabwe.

Siku ya tar 18 Agosti Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Anthipas Lissu, alitoa taarifa kuwa kuna mali za Tanzania zimezuiliwa nchini Canada kutokana na deni ambalo serikali inadaiwa na kampuni ya ukandarasi.

 Baada ya taarifa hizo kutolewa na mbunge huyo, serikali ikathibitisha uwepo wa suala hilo na kuongeza kuwa kuna ya watu  wa vyama vya upinzani wameshirikiana na makampuni ya nje kufungua kesi kama hizo, ili kuweka vikwazo kwa serikali kuweza kufanikisha mipango ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zito kabwe ni (timokrasi) mnafiki na ni miongoni mwa waliokuwa wakipinga kwa nguvu zote kununuliwa kwa ndege hizo. Lakini baada ya kuja kwa ndege mbili na kuonyesha mafanikio makubwa katika kutoa huduma ndipo Zito na wafuasi wake vikawashuka. Lakini hao akina Zito walipoona wameibika kqenye kuziekea figisu ndege hizo ndipo walipowapa mchongo hao wataliana kwenda kuweka madai yao kwenye hiyo ndege ili iwathibitishie watanzania kuwa wao waliokuwa wapo sshihi katika kupinga ndege hizo . Hebu jiulize Tanzania ina mali nyingi tu nje ya nchi tena mali zisizoondokeka kama nyumba za office za kibalozi nakadhalika iweje iwe ndege tu? Sababu Maghuful kaahidi ataleta ndege ikifika julai basi katika jitihada za kutaka kumpaka matope yeye na serikali yake ndio wanasiasa wa ndani wakatengeneza hilo zengwe. Sasa vioja gani anavyodai Zito kutoka kwa serikali kama sio yeye mwenyewe ndio kioja? Ni jitihada za kumuhujumu Maghuful lakini tujiulize kwa manufaa yanani?

    ReplyDelete
  2. Zito kabwe ni (timokrasi) mnafiki na ni miongoni mwa waliokuwa wakipinga kwa nguvu zote kununuliwa kwa ndege hizo. Lakini baada ya kuja kwa ndege mbili na kuonyesha mafanikio makubwa katika kutoa huduma ndipo Zito na wafuasi wake vikawashuka. Lakini hao akina Zito walipoona wameibika kqenye kuziekea figisu ndege hizo ndipo walipowapa mchongo hao wataliana kwenda kuweka madai yao kwenye hiyo ndege ili iwathibitishie watanzania kuwa wao waliokuwa wapo sshihi katika kupinga ndege hizo . Hebu jiulize Tanzania ina mali nyingi tu nje ya nchi tena mali zisizoondokeka kama nyumba za office za kibalozi nakadhalika iweje iwe ndege tu? Sababu Maghuful kaahidi ataleta ndege ikifika julai basi katika jitihada za kutaka kumpaka matope yeye na serikali yake ndio wanasiasa wa ndani wakatengeneza hilo zengwe. Sasa vioja gani anavyodai Zito kutoka kwa serikali kama sio yeye mwenyewe ndio kioja? Ni jitihada za kumuhujumu Maghuful lakini tujiulize kwa manufaa yanani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. tena hilo ni rinafiki sana na ndiyo maana hata kwao hawalipendi kwa ajili ya unafiki wake na huyo ni mmoja kati ya wanaowapa nguvu hao wanaojidai kwamnba wanaidai tanzania, ajiangalie sana na nitashangaa kigoma mjini mkimrudisha tena kwenye ubunge. mjinga sana huyo

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad