Zitto Kabwe Ajihami na Polisi Asema Atahakikishwa Akamatwi

Zitto Kabwe  Ajihami na Polisi Asema Atahakikishwa Akamatwi
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali, atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.

Akiwajibu wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.

“Sitaki na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria mpaka ndoto zao zilipotimia.

“Kagame alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa, Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka 36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.
Hivi karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.




Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jitto unaota mchana dogo. wewe na kagame au melisi wapi na wapi!!!

    ReplyDelete
  2. Angli feci...!!! unaanza tena? Tulikwisha pumzika na wewe .
    nilisha mwambia Mtatilo na Hehch sasa shauli yako.
    Wanakumindi...Halafu watakupa keshi.
    You need to Go Back to Skuli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad