Ziito Kabwe Kupitia Facebook Ameandika:
Bei ya Ndege moja aina ya Bombadier Q400 ambazo Tanzania ina/menunua ni USD 31m. Deni tunalodaiwa pamoja na riba ambalo Serikali imekiri na kuahidi kulipa ni USD 37m.
Hivyo Serikali yetu ingeweza kununua Ndege nyengine mpya iwapo ingeshughulikia vema kesi ya kampuni iliyoshikilia Ndege yetu. Hasara za namna hii ndio hurudisha nyuma Serikali za Afrika kwenye juhudi za Maendeleo.
Jambo la kushangaza ni pale Mbunge mwenye mamlaka ya Kikatiba kuihoji Serikali anapotimiza wajibu wake anakamatwa na kushtakiwa Kwa ' kutaja makosa ya Rais hadharani '. Sasa Mbunge ataje makosa ya Rais chooni? Chumbani? Shimoni? Mbunge wa Upinzani ni lazima ataje HADHARANI makosa ya Kiongozi wa Serikali ya Chama kinachoongoza dola.
Kazi ya Upinzani ni kuhoji. Ni kazi ya kimantiki na ya kikatiba.
Sahihi.Uongozi wetu ni wa kubabaishia tu.
ReplyDeleteSawa Sawa zito tuko pamoja
ReplyDeleteZito kabwe kumsapoti Tundu Lisu alichokisema ni sawa na shetani kusimamia kesi ya Iblisi .
ReplyDeleteMimi nnavyo mjua Zotto na tundu bovu hawapikwi chingu kimoja..KULIKONI?
ReplyDeleteSI NASIKIA ALIUZA VIWANJA KIGAMBONI NA SSNF NA ECROWS AKATIA NDANI.
ReplyDeletePIA ULIKUWA MGAO ULEEE. SETHMALILA