Abiria Aliyetamka ‘Allah Akbar’ Asababisha ndege Kuchelewa Kuondoka Airport

Abiria tisa wamezua taharuki kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Zaventem, nchini Ubelgiji baada ya mmoja wao kutamka matamshi yaliyosikika ‘Allah Akbar’ kwa sauti kubwa mara kadhaa.

Watu hao tisa walitolewa na maaskari kwenye ndege ya shirika la Ryanair, na kuamriwa mizigo yao kutolewa kwenye ndege ili kukaguliwa zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya ndegehiyo  kuondoka.

Ndege hiyo ililazimika kuchelewa kwa masaa manne ikipisha ukaguzi wa mizigo ya watu hao, ambao walitambuliwa kuwa ni raia wa Ubelgiji.

Polisi mjini Brussels wamethibitisha taarifa hizo kupitia kituo cha Runinga cha VTM Nieuws kwa kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi Tarehe 2 Septemba ambapo wavulana hao tisa walikuwa wanasafiri kutoka Mjini Brussels kwenda Madrid, Hispania.

“Tumepokea taarifa hizo za wanaume tisa waliokuwa wakisafiri kutoka Ubelgiji kwenda Madrid, Hispania lakini walipoingia kwenye ndege mmoja wao akaanza kutamka kwa sauti ‘Allah Akbar’ akimaanisha ‘Mungu mkubwa’ kama mara sita hivi ndipo askari wa usalama wakamtoa kwenye ndege pamoja na wenzake wote kwa ukaguzi”,amesema Peter De Waele msemaji wa jeshi la Polisi mjini Brussels .

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Top 24   abiria walioshuhudia tukio hilo wamesema lilitokea baada ya ndege hiyo kuchelewa masaa matatu kuruka na ndipo mtu huyo akaanza utani akitamka ‘Allah Akbar’ huku akicheka.

Hata hivyo abiria hao nane walirudishwa kwenye ndege baada ya ukaguzi kufanyika na ndege kuendelea na safari yake, ingawaje mpaka sasa bado haijawekwa wazi sababu za kupekuliwa kwa watu hao kwa mara ya mbili huku mitandao mingi duniani ikiandika kuwa ni hofu ya ugaidi iliyotanda nchini Ubelgiji.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sio ajabu ni watu wasiomjua ALLAH.NA KUTOMUAMINI.JE WANGESEMA HARE KRISHNA AU JESUS.Wangepekuliwa?
    kila watakapotaka kuziba au kupoteza nuru ya KIISLAMU NDIO INANGAA ZAID.ndani ya ndege hiyo watu wangapi wametamka Allahu Akbar baada ya tokeo hilo?
    ALLAHU AKBAR DAIMA NA DAIMA MPAKA SIKU YA MWISHO

    ReplyDelete
    Replies
    1. NANI WANAOZIBA NURU YA KIISLAM????????????

      Delete
    2. Jiulize kwanini mlipuko wowote wakigaidi unaofanywa nawasio waislamu hawatajwi Dini Zao.ila akishukiwa mtu anajina la kiislamu mara mmoja Wanatajwa waislamu wote.hii ni dalili mojawapo ya kutaka dini hii ichukiwe na hawatafaulu.

      Delete
  2. kwani kusema Mungu Mkubwa kosa? hawana akili hata moja hao askari Mungu awalaani

    ReplyDelete
  3. Hao wazungu ni wanafik kwani kusema alah akbar ndio ugaidi hawajiamini maana wanajua kuwa mungu yupo

    ReplyDelete
  4. Sio hivyo. Kwanza Lugha kwa binadam ni mgongano, Mataifa ya ulaya, Wageni wameingia wengi si muda mrefu, Wengine labda hawaelewi maana yake. Au labda ndiyo ile falsafa ya Wewe Miami. Mfano nchi za magharibi Ilishazoeleka Imani hii na nchi za mashariki ilishazoeleka Imani hii arimladi tu kila kitu kinatofautia huyu hivi yule hivi. Nadhani ukitamka jina la yesu kwenye nchi za masharaka utakuwa umekiuka sheria. Pengine waweza chukuliwa hatua, Kwa maana watasema umewakwaza watu wengi wa Taifa hili ni waumini wa Imani hii, kwanini. Usingeutumia huo muda kuomba ukiwa nyumbani kwako kuliko kuja kwenye alaiki ya watu na kuwapigia kelele. Ndivyo mambo yalivyo, angalau nchi za mangaribi zina uvumilivu na busara, hata mtu atamke kwa luhga yake na Imani yake hamna mtu atakaye shughulika na Wewe. Alimradi ni Imani yako na unamuomba Mungu. Ni uhuru wa kuabudu kwa muumba, hili tukio Nadhani ni kwa kuwa labda walikuwa na hofu ya magaidi kumbe wakati walaaa Sio. Sio binadam wote wabaya au Sio wote wazuri, wawe wa Imani yoyote ile au wa rangi yoyote hile, kwani wazuri na wabaya wote wapo humo humo.

    ReplyDelete
  5. Hii si dini ni mpango wa shetani. Dini gani imeua hivi. allah is dead... his followers are blind

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni KAFIRI na hujui ulisemalo. Nyinyi makafiri ni woga wa KUFA na ndio maana hamjiamini. ALLAH atakusaidia usilimu haraka kwa uwezo wake. Waislamu wao wanajua kufa ni jambo la kawaida na ni lazima. Muislamu yeyote hana uhakika wa kufika dakika moja ijayo. Wewe ripua mabomu utakayo kama ALLAH hakuandika wewe ufe muda ule basi hufi. na jiulize wangapi wamekufa kitandani na wangapi wamepona vitani?

      Delete
  6. WEWE ANONYMOUS5 SEPTEMBER 2017 AT 14:40
    "Hii si dini ni mpango wa shetani. Dini gani imeua hivi. allah is dead... his followers are blind"HAKIKA WEWE NDIYO BLIND.-HUJUI ULISEMALO WALA ULIJUWALO KAMA WEWE WAZAZI WAKO BABU NA BIBI ZAKO NA GENERATION YAKO YOOOOTE TANGU PALE NABII MUSSA as ALIPOPAZWA MBINGUNI NA MWENYEZI MUNGU NA sio kuuawa na bali kufananishiwa na mtu aliyefanananae tu.km yeye mwenyewe nabii MUSA as baada yangu atakuja ahmad yani mtume MOHAMMAD saw. Yeye atakuwa mtume wa viumbe wote akimaanisha binadamu wanyama wadudu ndege na kila kilicho ktk dunia na mbigu..HAYA SEMA SASA WEWE WA DINI GANI????NA HYO MANENO ALLAH AKBER-MWENYEZI MUNGU MKUBWA, na salamu za huko akhera ni ndiyo hii unayoisikiaga hapa duniani"ASALAAM ALEIKUM,..NENDA KASOME BIBLIA AGANO LA KALE..

    ReplyDelete
  7. ANONYMOUS5 SEPTEMBER 2017 AT 14:40 "Hii si dini ni mpango wa shetani."CHUKULIA MFANO MDOGO TU..KWENYE FAMILIA YENU MKO WANGAPI-SASA BAADHI AU MMOJA WENU AKIWA MCHAWI AU SHOGA AU NYONYA DAMU UTAMLAUMU BAB NA MAMAKO..LA HASHA WAZAZI HAWANA MAKOSA HASILANI LAO NI KULETA ULIMWENGUNI KUKULEA KUKUKUZA MPAKA UKAPATA AKILI UKACHAGUA KUWA KM NI SHOGA,MWANGA nk.kwa maana DINI hii ni km WAZAZI..NAKUBWA AU BAYA ZAIDI MDOGO WANGU MPAKA NAKUURUMIA KWA KAULI YAKO "allah is dead..."WE MTOTO humuogopi MUNGU,Haya kawaulize akina FILAUNI wa pale Egipty alivyo laaniwa na MWENYEZI MUNGU saa Kwa kauli zake tu..km yeye Filaun ni mungu mkubwa na makufuru,misifa mingine mingi..M/MUNGU AKAMWAPISHA kamwe ardhi haitamstiri mpaka siku ya kiama atabakia vile vile watu wamuone huyo alojifanya yeye ndo mungu mkubwa ,mbona amekufa.kwa maana M/MUNGU hafi wala hashikwi na usingizi mwenye kutoa riziki kwa viumbe woooooote mbinguni na ardhini binadam,wanyama wadudu ,mimea nk...kwa HAKIKA HILO LAKO "allah is dead..."NI KUBWA MNO ZAIDI...kazi ya msamaha unayo mdogo wangu tena sio wa kitoto seriously..omba toba ilokuwa nzito wa husirudie tena na kauli km hizo..utaangamia...KWA KIFUPI TU NIseme umshukuru mtume MOHAMMAD saw.ALIMUOMBA MMUNGU sw HASITOE HUKUMU YA PAPO KWA PAPO KWA UMMATI WAKE WOOOTE AMBAO NI MIMI NA WEWE NA WANYAMA WADUDU AKINA NDEGE nk.mpaka lini kaburini-POLE SANA..NA HAO WANAOTUMIA KIVULI CHA DINI HII YA KIISLAM KAZI WANAYO KUANZIA MAKABURINI MWAO...nazani utakuwa umenielewa....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad