Ahukumiwa Miaka 30 Jera kwa Kosa la Kubaka na Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Miaka 13

Ahukumiwa Miaka 30 Jera kwa Kosa la Kubaka na Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Miaka 13
MAHAKAMA ya wilaya ya Lindi, imemtia hatiani na kumuadhibu kwenda gerezani na kutumikia adhabu ya kifungo kwa muda wa miaka 30, kijana anaetambulika kwa jina la Mussa Saidi, mkazi wa mtaa wa Mitandi manispaa ya Lindi. Baada ya kuthibitika kuwa alimbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 13.

 Akisoma hukumu ya shauri hilo la jinai namba 110 la mwaka 2017, hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Erasto Philly alisema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na pande zote mbili (upande wa utetezi na mashitaka) mahakama hiyo iliridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka. Kwamba Mussa alimbaka na kumpa mimba mtoto huyo ambae kwa mujibu wa maelezo ya mwendesha mashitaka wa serikali, EmmanueJohn, ni mtoto  wa mke wake Mussa(mtoto wake wa kambo).

Hakimu Philly alisema ushahidi uliotolewa dhidi ya Mussa mahakamani hapo haukuwa na chembe hata ya shaka kuwa Mussa alitenda makosa hayo ambayo yapo kinyume na sheria za nchi nayamekatazwa kutendwa na mtu mwenye akili timamu kama Mussa.

Kwakuzingatia ukweli huo, hakimu Philly alisema mahakama hiyo ilimudhibu adhabu ya miaka 30 kwa kosa la kubaka. Ambalo ni kinyume cha sheria namba 130 vifungu vya 1 na 2 (1) cha sheria ya adhabu sehemu ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Vilevile kwakosa la kumjaza mimba mwanafunzi, mahakama hiyo ilimuadhibu miaka 30,ikiwa  utekelezaji wa sheria ya elimu ,kifungu namba 60A(3) cha sheria hiyo fungu la 553 kama lilivyorekebishwa mwaka 2002 na marekebisho mengine ya pili yaliyofanyika mwaka 2016.

Huku akiweka wazi kwamba utekelezaji wa adhabu hiyo utafanyika kwa pamoja.Hivyo Mussa atatumikia adhabu hiyo kwa muda wa miaka 30 pekee. Lakini  pia hakimu huyo alisema mahakama kwakuzingatia ukweli kwamba mtoto amekatizwa masomo. Mussa ametakitakiwa kumlipa  shilingi 1,000,000/= kama fidia.

Awali mwendesha mashitaka wa serikali,Emmanuel John aliileza mahakama hiyo kwamba mwezi Agosti mwaka huu akiwa nyumbani kwake mtaa wa Mitandi alimbaka na kumsababishia kupata mimba mtoto huyo mdogo wa kike ambae ndoto zake za kufika mbali kielimu zimekatizwa bila kutarajia. Hivyo aliiomba mahakama hiyo imuadhibu adhabu kali ili iwefundisho kwa wengine wanaotamani kutenda makosa ya aina hiyo.

Mussa licha ya kuiomba mahakama imuhurumie kwa kumpa adhabu ndogo kwakuwa hanarekodi mbaya ya kutenda makosa,ana wazazi,make na watoto ambao wote wanamtegemea. Hata hivyo kiwango,muda wa kutumikia na aina ya adhabu vilibaki kuwa hizo na kusababisha kuwa gumzo kutoka kwa watu wanaofahamu na wasiomfamu kijana huyo hapa Lindi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad