Ally Hapi Aagiza Kupitiwa Upya Mkataba wa Mwekezaji wa Kituo cha Mabasi cha Makumbusho

Ally Hapi Aagiza Kupitiwa Upya Mkataba wa Mwekezaji wa Kituo cha Mabasi cha Makumbusho
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameagiza kupitiwa upya kwa mkataba wa mwekezaji katika Kituo cha mabasi cha makumbusho baada ya kubaini kuwapo kwa ubadhirifu.

Mkataba huo ni kati ya Manispaa ya Kinondoni na Kampuni ya Eastern Capital Limited kwa ajili ya kuendesha kituo hicho.

Akiwa ziarani hapo  leo, Hapi ameelezwa na wafanyabiashara wakiwamo bodaboda,  bajaji na machinga kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiwalipisha kodi kubwa na michango bila kuwapa risiti wala kutoelezwa matumizi ya tozo hizo.

Hapi alitaka kupata ufafanuzi wa kina kwamba  fedha hizo zinapelekwa Manispaa na kama wanatoa risiti za EFD lakini haikuwa hivyo.

"Ni marufuku kukusanya fedha nje ya mkataba, kinachokuongoza ni mkataba sasa nataka kujua hicho unachotoza kama hakipo kwenye mkataba nani aliyekutuma?,"

"Namuagiza Mkurugenzi wa Manispaa, apitie upya mkataba  huu na kama hauna tija uvunjwe," amesema

Ametoa siku tatu kwa Kampuni hiyo kutoa taarifa za makusanyo ya fedha pamoja na kueleza kiasi cha kodi walicholipa tangu kuanza kwa mkataba.

Meneja miradi wa Kampuni hiyo, Haidary Salum amesema makusanyo na tozo zikiwamo usafi, umeme na ulinzi ulitokana na makubaliano kati yao na wafanyabiashara.

" Ndiyo haipo kwenye mkataba lakini tulikubaliana na wafanyabiashara ili wachangie huduma,"amesema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad