Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.
Askofu Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.
Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.
Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.
Askofu Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.
"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."
Amesema anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.
"Rais anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”
"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."
Amesema, "Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu, ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi."
Kuna nguvu toka nje ya nchi inaunga migogoro hii kwa maslahi yao ya uwekezaji nchini. Hawa wawekezaji hawajali maslahi ya nchi hii, hawajali maslai ya Watanzania, ingawa tunapitia hali ngumu kisiasa, kwa kweli mataifa makubwa bado yanatoa sifa kubwa na kuipongeza serikali hii sababu, wameichagua Tanzania kuwa ndiyo uwekezaji wao mkuu unalenga. Na wanatumia mitengano na misukosuko yetu kupenyeza haja zao. Wameisifia Africa hasa tanzania kuwa ndipo sehemu nzuri na rahisi kujitengenezea pesa. Haya matangazo yametokea UN, na nchi za kibepari. Tanzania imevamiwa kwa uwekezaji kutumia sintomfahamu ya siasa na serikali yetu tawala. Ninachokiona hapa, mazingira magumu kwa Watanzania na rahisi kwa Wawekezaji. Haitapita muda tutaona wimbi kubwa tena la Uwekezaji bila sheria za kinga na misukosuko kama hii tunayoipitia sasa. Ni katiba ya nchi tu itatukinga Watanzania na kutulinda. La nchi imeuzwa tena wakati watu wanamsifia Raisi kutoa ufisadi ambapo si kweli. Ni ufisadi wa hali ya juu toka nje unaingia kwa kasi kubwa huku tukiuana sisi kwa sisi. Inasikitisha sana watu wa uchumi wetu wako bizzy kutafuta wawekezaji kila kukicha bila kuyaweka mazingira safi, na Wazi kwa wahusika wa nchi hii kwani wengi wao bado wapo gizani wakimpigia makofi Raisi. Ni jukumu kubwa kwa Wapinzani wote nchini kuungana kwa pamoja na kuacha kuangalia itikadi. Ni muhimu sana kuungana kuliokoa Taifa letu huku linakoelekea. Ni vizuri sana ingawa kuna wasomi wa juu lakini mwamko wao finyu kwa jambo hili, lakini naamini kuna wengi wao wanaelewa lakini wanafungwa midomo kila kukicha. Kuna wengi pia toka CCM wanaliona hili, je Kwa nini kwa mara ya kwanza katika Taifa watu wakakutana wenye mawazo na msimamo moja, kwa pamoja wakadai katiba mpya kwanza, na kuamua kwa pamoja hakuna uwekezaji mpaka nchi iwe na kauli moja?Na yeyote mwekezaji anayekuja ajue wazi hana protection kwa sasa.Kwani kuna mpasuko.Watu wanaingilia kote upinzani na chama tawala kuharibu nchi hii.Si wengi wenye utashi na kutakia mema nchi yetu. Wako kwa manufaa yao tu. Tunaukubali ubepari si asilia yetu. Ni nchi yetu tu kuna undugu, mabepari kwao hakuna kitu kama undugu. Wao wako tayari kuunganisha nguvu kipesa na kisilaha kuja kutengeneza pesa na utajiri zaidi na kujipa nguvu zaidi kiuchumi kupitia nchi zetu.Je, hakuna wanohitaji uwekezaji kwao? MMeona vimbunga na wengi wanahitaji misaada. Hamjifikirii inawezekanaje sisi nchi ya Adrica, waitayo maskini, tukawa watu wa kwanza kutujali. Kuna kitu kikubwa wanakihitaji huenda wameshakishikilia au karibu wanakimiliki chote kabla hatujaamka. Mtanzania yeyote, mzalendo, mwenye mapenzi na nchi hii na watu wake, hawezi kukubali nchi na utajiri wa watu watanzania unyan'ganywe wote na watu wa nje naswerevu wachache nchini, huku tukiambiwa tunatumbua ufisadi.Hatuwezi kukubali kwa watu wachache wanaotuambia hii maiti zinazookotwa ni wakimbizi toka Ethiopia,.hatuwezi kukubali viongozi wetu washikwe majukwaani wakitenda kazi zao za kutoa elimu kwa Wananchi na kusikiliza shida za wananchi. Taifa letu ni teule lililojengwa kwa misingi ya utu, upendo, jamii, usawa haki na ushirikiano. Tuvitunze hivi na tusikubali mtu yeyote kwa sababu ya pesa na nguvu za silaha tuwe vibaraka vyao.Utu wa kila mtanzania uthaminiwe Tafadhali. Hakuna nchi hata moja itakayomthamini Mtanzania kama nyumbani. Tusigeuzwe wageni nyumbani kwetu. Inauma.
ReplyDelete