Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amewataka watu waovu watambue kumuondoa Tundu Lissu mmoja kutazalisha Lissu wengine maelfu.
Kauli ya Askofu Shoo inatokana na kuchukizwa na jaribio lililoshindwa la kumuua Lissu Alhamisi iliyopita mjini Dodoma, ambapo watu waliokuwa na silaha walishambulia gari lake kwa risasi 32.
Katika shambulizi hilo, kati ya risasi hizo 32 zilizofyatuliwa, risasi tano zilimpata Lissu maeneo mbalimbali ya mwili wake, na sasa anatibiwa katika hospitali ya Aghakhan ya Jijini Nairobi,Kenya.
Akizungumza kutoka Bonn Ujerumani leo , Askofu Shoo ametoa wito maalum kwa Serikali ya Rais John Magufuli, kuhakikisha wote waliohusika na unyama huo wanakamatwa.
“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa za kupigwa risasi Mheshimiwa Tundu Lisu. Watanzania tunapaswa kukataa na kulaani kwa nguvu zote vitendo kama hivi,”amesema na kuongeza;-
“Mimi ninaamini kuwa nguvu zile zile za uovu zilizokuwepo tangu awamu zilizotangulia ndizo zinazoendeleza unyama kama huu. Ninamwomba Mungu ampe (Lissu) uponyaji wa haraka”.
“Tundu Lissu amekuwa mstari wa mbele kufunua ufisadi unaoendeshwa na wababe wachache. Hawa wanaona sasa wameanza kutikiswa, na kwa kuwa kwao wingi wa mali na pesa ndio mungu wao”
“Hatushangai wakitumia kila njia kuzuia ufisadi wao usianikwe hadharani. Watajaribu kila njia kuzuia ukweli lakini wanasahau kuwa ukweli hauzuiliki milele kuna siku utajitokeza tu”.
“Kumwondoa Lissu mmoja kutazalisha Lissu maelfu. Wito wangu kwa serikali ya Dr Magufuli ni huu, kwamba watu wote waliohusika wasakwe na wafikishwe mbele ya sheria,”.
Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT amesema Serikali yoyote makini inajua namna ya kuulinda upinzani kwani ukitumika vizuri unakuwa kioo cha serikali cha kujitazama.
Mara kadhaa, kiongozi huyo amekuwa akitoa hotuba zenye hisia kali akitaka Serikali na vyombo vyake vya usalama kuchukua hatua, kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ajabu ya kihalifu.
Mwananchi
makufuli na serikali yake itakuwa wameunda kikundi maalum cha kuwanyamazisha watu wanaoikosoa serikali.mambo yanayotokea nchini sio ya kiutu, watazania msipo angalia huyu Rais atatupeleka pabaya, utulivu na amani iliyotengenezwa kwa miaka mingi asije akaipoteza, na wala asijifanye Mungu mtu, madaraka ni zamana yasimleweshe. inaelekea anafanya mbinu za Kagame. MUNGU Atamlani wote aliohusika.
ReplyDeleteHuyu Askofu kama mchepuko fulani hivi na wala hajui anachokiongea zaidi ya mawazo ya kimhemko na kishabiki. Kama Askofu nadhani angepaswa kufahamu yakwamba muovu au waovu kama alivyosema huwa hawangalii litalokuja baadae kwani tayari ni tayari waovu cha kufanya yeye kama askofu ni kuwaombea hao waovu warudi na kuwa watu wema badala ya kutoa kauli ya kuhamisha kazalisha watu zaidi wenye fitna kama Lisu. Bila ya yakuwa na mtu kama Lisu katika jamii ya watanzania tusingefika hapa tulipofika kwenye taifa linalojulikana kama kisiwa cha amani Africa. Na Hakuna ushaidi wowote unaonyesha yakuwa serikali imehusika na tukio la Lisu. Isipokuwa yeye mwenyewe Lisu kabla hata hayajamfika yaliyomfika alikuwa akitafuta kiki za makusudi kwa serikali eti Lisu kiboko ya Maghuful? Upumbavu mtupu kwanini isiwe Lisu kiboko ya maendeleo huko jimboni kwake? Maghuful ni kiboko kwa maendeleo ya Tanzania na watanzania. Na yeyote anaemuombea mabaya basi Mungu atamuangamiza yeye kwanza. Yeyote anaemuombea mabaya Maghuful ni adui wa nchi yetu na Mungu atamuangamiza ampe laana apotee kama moshi unavyotoweka angani Amin.
ReplyDelete