Baba; Mtoto Wako Mtundu, Amekunya Mkononi, Je, Utaukata au Kuusafisha na Kumsafisha?

Huu ni uzi wa swali la hypothetical situation kuhusu wewe kama Baba wa Familia, Mtoto Wako Mtundu, Amekuny.a Mkononi, Jee Utaukata Mkono, au Utausafisha na Kumsafisha?.

Baba ukiachiwa mtoto, halafu akikuny.a mkono, hauukati, wala humchapi mtoto, bali utausafisha mkono, na utamsafisha mtoto na kuendelea kumbeba.

Rais wa nchi ni kama baba, rais wote wa Tanzania ni kama watoto, hata wakikunye.a mkono, haupaswi kuwachapa, kuwasusa, bali kuwakumbatia na kuwa support.

Hata kama taratibu zimekiukwa, lakini huyu ni mtoto wa Tanzania, ni Mtanzania mwenzetu, kwa vile alikuwa very vocal kumhusu baba na serikali yake, baada ya kushambuliwa, mtu yoyote lazima angehofia uangalizi wa baba kwa hisia kuwa ni hasira za baba, hivyo wako very right, kwenda mahali salama.

Lakini despite all, serikali yetu bado has a duty of care, Bunge letu bado has a duty of care kumhudumia na kugharimia matibabu na ikibidi kutoa support ahamishiwe kwenye nchi yenye matibabu bora zaidi.

Kunyoosha huku mikono kutoa support, ni unconditional and despite all the odds kwa sababu kila mzazi has a duty of care kwa watoto wake regardless of anything!.

Ifike mahali, viongozi wetu, waogope kitu kinachoitwa karma, ambapo wewe kama ni kiongozi, ni kama baba, you have a duty of care kwa raia wako wote, if there is anything you can do to help out, please do!, tena do it now before its too late!.

Karma inaelekeza, if there is something bad that has happened to someone, uwe unahusika, a huusiki, but there is something you can do to help out, but you don't do kwa sababu tuu taratibu hazikufuatwa, au kwa sababu unanyooshewa kidole, karma inaelekeza just ignore everything, maneno, vidole na taratibu zilizokiukwa, just do what you can do to help out. Mtume balozi wetu pale aka assess the situation and if there is something you can do, please do!.

Kwa sababu, if something will happen, kwa sababu you didn't do anything to help out, na ulikuwa na uwezo wa kusaidia na kuzuia hiyo something is happen, then, the karma of what happens will also be upon you kwa kushindwa kutimiza wajibu wako kumhusu raia wako!.

Hii karma jamani haijui nani ni nani, wala haijalishi mamlaka ya kidunia hii, karma is real, tutimize wajibu wetu ipasavyo kuepuka a bad karma, kwa kutenda mema, hata kwa wabaya wetu, ili kujenga karma njema.

Namalizia kwa swali hili, Jee Wewe Kama Baba, Mtoto Wako Mtundu Sana, Akikuny.a Kwenye Mkono, Jee Utaukata?, Utamchapa?, au Utamsusa?, au Utausafisha na Kumhudumia kwa Kumsafisha?.

Get Well Soon, TL.

By Pascal Mayalla

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad