Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhidi ya benki hiyo, wakiilaumu benki hiyo kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha ambapo pesa hizo zilitumiwa kununua silaha na kukiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC linasema, Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo, Theoneste Bagosora, anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalitokea baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu kudunguliwa Aprili 6, 1994.