Benki Iliyohusika na Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda Yachunguzwa

Benki ya Iliyohusika na Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda Yachunguzwa
Nchi ya Ufaransa inadaiwa kuanzisha uchunguzi dhidi ya benki ya BNP Paribas, kufuatia madai kuwa ilihusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.

Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhidi ya benki hiyo, wakiilaumu benki hiyo kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha ambapo pesa hizo zilitumiwa kununua silaha na kukiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC linasema, Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo, Theoneste Bagosora, anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalitokea baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu kudunguliwa Aprili 6, 1994.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad