Kwe-nye maho-jiano haya maal-umu ambayo mwa-ndishi wetu ame-fanya naye uso kwa uso nyumbani kwake, Bunju jijini Dar, utapata majibu ya maswali yako, songa nayo;
Swali: Habari yako Bi. Cheka, naona upo kimya vipi muziki umeacha?
Bi. Cheka: Naanzaje kuiacha fani yangu? Muziki upo kwenye damu, bado ninafanya ila tu watu hawajui.
Swali: Nakumbuka kuna kipindi ulikuwa na mgogoro na Fella, alikuahidi kukujengea, akakutelekeza, mliishia vipi?
Bi. Cheka: Sina tatizo naye, alinipa matofali kadhaa ya kujengea hii nyumba, mengine nikaongeza mwenyewe. Sitaki kumuongelea sana kwa sababu sipo kwake, nilivunja mkataba, ulikuwa wa miaka mitano, nikafanya minne.
Swali: Baada ya hapo hakukwambia kama anataka aendelee ‘kukumeneji’ na ikitokea akakwambia hivyo, je, utakubali?
Bi. Cheka: Ni kweli ninahitaji meneja wa kusimamia kazi zangu, lakini sipo tayari kurudi kwake kwa sababu tulishindwana.
Swali: Ni changamoto gani unakutana nazo katika kipindi hiki ambacho huna meneja?
Bi. Cheka: Kuna ugumu, ila ninashukuru Mungu kuna kijana anaitwa Jophrey aliniafanyia bure video ya ngoma yangu ya Cheka Bella Pansupansupa ambayo itatoka hivi karibuni.
Showbiz Extra: Kuna tofauti gani kwenye maslahi unavyofanya shoo sasa na ilivyokuwa kipindi cha nyuma wakati upo kwa Fella?
Bi. Cheka: Tofauti ipo japo siyo kubwa sana, kwa kuwa pesa ninayolipwa sasa sigawani na mtu.
Showbiz Extra: Unawezaje kujikimu kimaisha, kuna kitu unafanya mbali na muziki?
Bi. Cheka: Sina biashara yoyote, kinachopatikana siku zinaenda japo ninasumbuliwa na miguu, muda mwingine inavimba, ndo’ inanitesa kwenye matibabu, lakini hainizuii kufanya shoo.
Swali: Kuna baadhi ya wanaume wanaona fahari kutembea na watu maarufu, hakuna mtu alitejito-keza kukuoa?
Bi. Cheka: (Kicheko) wapo hao, kuna mmoja nd’o aliniacha hoi, alitaka anioe mke wa tatu na kuniahidi mambo kibao ikiwemo kunijengea na kunipa gari, nikakataa hivyo ninaishi mwenyewe na wajukuu wangu
Swali; Unazungumziaje soko la muziki kwa sasa?
Bi. Cheka: Hivyohivyo tu, naona wasanii wengi siku hizi muziki wao wanawaza kupondana tu kuliko kujali ubora wa kazi.
Swali: Ni mwanamuziki gani unamkubali kwa sasa?
Bi. Cheka: Nampenda sana Ali Kiba, kwa sababu muziki wake anaofanya ni wa kipekee, siyo wa kumuiga mtu, kama mimi ninavyofanya muziki wa peke yangu, pia ni kijana mstaarabu, hana mashauzi kama wengine, ananijua vizuri na hajawahi kuniringia, hiyo ndiyo sifa ya msanii.
Swali: Unazungumziaje kitendo cha wasanii kuvaa utupu jukwaani, inasaidia kufanya shoo kwa uhuru au ndo’ mambo ya kizungu?
Bi. Cheka: Ushamba tu unawasumbua, siyo lazima ukae uchi jukwaani ndo’ uonekane mjanja, siku hizi wamezidisha, wabadilike.
Swali: Mashabiki watarajie nini kutoka kwako?
Bi. Cheka: Watarajie kazi nzuri kutoka kwangu, sijafa, nikifa watasikia, wanipende na kunisapoti.
Swali: Ahsante kwa ushirikiano.
Bi. Cheka: Karibu tena.