Bila Rais Magufuli Nchi Isingefikia Hatua ya Kupambana na Ufisadi wa Madini- Ndugai

Bila Rais Magufuli Nchi Isingefikia Hatua ya Kupambana na Ufisadi wa Madini- Ndugai
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai bila ya Rais Magufuli nchi isingeweza kufika katika hatua ya kupambana na ufisadi wa madini hivyo watanzania wanapaswa wamshukuru kwa kuweza kujitoa kusimamia rasimali za nchi bila ya woga.

Spika Ndugai amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya ripoti ya kamati ya uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili.
"Kumpata Rais aliyejitoa kusimamia rasimali za nchi si jambo rahisi wala jepesi. Mwalimu alijaribu kufanya hivyo awamu ya kwanza pakawa na tabu mtindo mmoja lakini watanzania walishikana naye kwa magumu yote yaliyokuwepo hadi mwisho kwa hiyo sasa lazima tushikamane na Rais wetu hata kama tunapo kwenda tutakuwa na magumu yeyote yale kwa maana kwamba lazima rasimali za nchi ziwafaidishe watanzania kwa namna moja ama nyingine, hatusemi asilimia 100 iwe yetu hatuwezi kwa sababu tunahitaji teknolojia, fedha na mambo mengine kutoka wa wabia wenye nia njema ili nasi tupate", amesema Ndugai.

Pamoja na hayo, Mhe. Ndugai ameendelea kwa kusema "ndugu zangu watanzania tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumpata Rais Magufuli, sisemi haya kwa sababu yupo mbele yangu, nyinyi wenzangu mnafahamu nchi zetu za Afrika hizi historia zetu za Afrika na jinsi tulivyokuwa tumeneemeshwa na Mwenyezi Mungu lakini wajanja wachache wanachukua mali za

Afrika na kuiacha haina lolote tangu wakati wa mkoloni na baada ya mkoloni", amesisitiza Ndugai.
Kwa upande mwingine, Mhe. Ndugai amewasisitizia wabunge kuwa na umoja katika mambo ambayo yanawaunganisha ambapo moja wapo ni kuhusu rasimali za taifa huku akipiga dongo kwa kusema wanaopaswa kukosa uzalendo ni Simba na Yanga kwa sababu wao wanaimba kabisa uzalendo umewashinda pindi wawapo uwanjani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad