Bondia Mayweather Akosolewa kwa Kumtetea Trump

Bondia Mayweather Akosolewa kwa Kumtetea Trump
Bondia Mmarekani Floyd Mayweather amekosolewa sana katika mitandao ya kijamii kwa kutetea maneno makali ya udhalilishaji wa wanawake ambayo yalitolewa na Donald Trump mwaka 2005.
"Anazungumza kama mwanamume halisi," Mayweather, aliyehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Bw Trump mwezi Januari, aliambia tovuti ya Hollywood Unlocked.

Ujumbe wake huo umekosolewa sana, huku baadhi ya wakosoaji wakirejelea visa vya awali ambapo bondia huyo alipatikana na makosa ya kuwadhalilisha wanawake nyumbani kwake.
Bw Trump aliomba rangi kwa matamshi yake hayo ambayo yalikuwa kwenye mkanda wa video uliofichuliwa mwaka jana.

Kwenye video hiyo, Bw Trump anasikika akijitapa kuhusu kuwapiga busu wanawake na kuwakamata kwenye sehemu zao nyeti, wakati wa mazungumzo ya faragha.
Mayweather ameambia Hollywood Unlocked kwamba Bw Trump "hakufanya jambo lolote mbaya".
"Wanaume halisi huzungumza hivi: 'Man, she had a fat ass. You see her ass? I had to squeeze her ass?' (Bwana, ana makalio mazuri. unayaona makalio yake? Ilinibidi kuyafinya makalio yake). "Mwanabondia huyo alisema.

"Kwa hivyo, anapiga gumzo la faraghani. Mazungumzo ya faraghani."
Wengi katika mitandao ya kijamii yalizungumzia historia ya Mayweather ya kuwashambulia wanawake.

Mayweather amewahi kutangaza kumuunga mkono Bw Trump, ambaye wakati mmoja aliwahi kumwelezea kama "mmoja wa mabondia bora zaidi kuwahi kutokea".
Mayweather pia alitetea Bw Trump kuhusu tuhuma za kuunga mkono makundi ya ubaguzi wa rangi.
"Haujawahi kusikia kuhusu Donald Trump kuwa mbaguzi wa rangi hadi alipowania urais," amesema Mayweather.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad