Mhandisi Kakoko ameyasema hayo Septemba 24 mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango alipotembelea bandarini hapo ili kupata maelezo kuhusu mchakato wa kupata mita mpya za kupimia mafuta (Flow Meters).
Kakoko amesema kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kimenasa wahalifu wakijiandaa kutoboa bomba na kuiba mafuta kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi.
Waziri Mpango amewapongeza askari wa doria waliofanikisha kukamata boti moja pamoja na vifaa vyake ikiwemo injini baada ya kuwadhibiti maharamia waliotaka kutoboa bomba na kuiba mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.