Chadema Msijifiche Nyuma ya Kivuli cha Supreme Court ya Kenya......

Leo majira ya mchana dunia ilishuhudia tukio kubwa zaidi la mahakama ya juu zaidi ya Kenya kuubatilisha uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 nchini humo.

Kwanini naliita tukio la kihistoria duniani? Ni kwasababu malalamiko ya kasoro za uchaguzi juu ya mfumo wa kidigitali yalishatolewa hata nchini marekani lakini walioshindwa nchini humo(chama cha Democrat) walishindwa kuchukua hatua ya kwenda kuhoji kwenye mahakama zao, kitu ambacho NASA ya Kenya ilithubutu.

Katika kuthubutu huko, watu mbalimbali hapa nchini kwetu walimbeza sana Raila Odinga, na wengine kumuita sore looser ambaye hajawahi kukubali kushindwa.

Lakini baada ya uthubutu huo, leo hii mahakama imetangaza kurudiwa kwa uchaguzi huo ndani ya siku 60.

KWANINI UAMUZI WA MAHAKAMA YA JUU YA KENYA UMEWAUMBUA CHADEMA? 

Inafahamika kwamba Ndugu Edward Lowasaa alifanya official endorsement kwa upande Raisi Uhuru Kenyatta, akishawishi kabila la wamasai nchini humo kumchagua Uhuru ili awe tena raisi wa kenya kwa mara nyingine.

Mara baada ya matokeo ya uchaguzi huo, bwana Lowassa alimpongeza ndugu Kenyatta kwa ushindi, tena akisisitiza kia uchaguzi ulikua wa Huru na wa Haki!!!

Mbaya zaidi wafuasi wengi wa Chadema, walilipuka mtandaoni na kushangilia ushindi huo wa kenyatta kwa kusisitiza kua uchaguzi huo ulikua wa "huru na haki".

Katika hali ambayo ni ya kushangaza, hata wasimamizi wa uchaguzi waliotokea nchi za ulaya nao walisema uchaguzi wa kenya ulikua huru na wa haki. Wasimamizi hawa baada ya tukio la leo tumeibua mambo mawili, kwanza, inawezekana walifahamu kua maslahi yao chini ya Kenyata yangelindwa vizuri au pili, hiyo dhana ya demokrasia na uhuru wa uchaguzi wanayoisema kua nchi za Afrika zinashindwa kusimamia haina uthamani wowote kwao hata itakapovunjwa, kwasababu sio rahisi kusema kua hawakufahamu kasoro hizo.

MAANA HALISI YA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI ALIYOKUA ANAIMAANISHA NDUGU LOWASSA NA WAFUASI WA CHADEMA.

kwa miaka mingi, kama sio yote, ndugu lowassa alikua ni mwanachama wa CCM, Chama ambacho kimelalamikiwa kwa manuva mengi waliyowahi kuyafanya kwenye chaguzi mbalimbali zilizopita.

Na ifahamike kwa ngazi aliyofikia ndugu lowassa alikua ni master mind wa magumashi mengi sana ambayo pengine hata wanachadema wengi wakigundua watabaki midomo wazi, au wanayajua ila hawana locus standi ya kuhoji kwasababu tayari yupo ndani ya chama chao.

Kwa maana hiyo kwa uzoefu wa umafia wa chaguzi alizowahi kushiriki akiwa kama sehemu ya chama tawala, uchaguzi wa uhuru na haki alioumaanisha ni uchaguzi wa magumashi na figisu ambao mahakama ya juu ya kenya imeufuta leo.

Kwa lugha rahisi tunaweza tukasema lowassa alirudia kwenye zama zake za umafia kama alivyokua enzi zake, au lowassa alikua kwenye sura yake halisi.

Na kwabahati mbaya sana wanachama wa chadema wakaingia kwenye mkenge huo wa kusapoti umafia.

Umafia ambao ulionekana dhahiri ni pamoja kuuwawa kwa mkuu wa tume ya uchaguzi kwenye maswala ya kimtandao huku akikatwa vidole na kuonekana ameingia kwenye akaunti yake ya kazini siku kadhaa baada ya kufa, nafkiri ni kwa kutumia vidole hivyo vilivyopotea.

Kwahiyo wanachama wa chadema wakajikuta wanashangilia umafia, ikiwemo damu ya marehemu msando chini ya kivuli cha uchaguzi huru na haki.

KINACHOENDELEA KWA SASA MITANDAONI. 

katika hali ambayo ni kushangaza, tena bila aibu, wafuasi wa chadema wanaipongeza mahakama ambayo imesema uchaguzi huo wa kenya ambao wao walisisitiza kua ulikua wa "huru na haki".

Kwa maana hiyo wanashangilia mahakama ambayo inabatilisha misimamo yao.

Mkenge ambao waliingizwa na mafia wa uchaguzi ndugu lowassa ni dhahiri umewaaibisha, umedhihirisha unafki wao.

Naomba kuwasilisha.

By Muwindaji/JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna cha ajabu hapo, chadema wao ni 'vigeu-geu' maisha yote, wanafuata uelekeo wa 'upepo'. Walimtukana Lowasa kuwa ni FISADI, MWIZI, wakaapa kabisa akina tundulisu kwamba wakishika dola 'WATAMFUNGA JELA'.....kama kawaida yao kwenye uchaguzi 'wakageuka' eti Lowasa huyo huyo mwizi,fisadi akawa 'malaika'!! Wakampigia debe bila haya eti awe rais hahaha, badala yake akawa 'rahisi'....hiyo ndio "chadema ya mbowe" mwenyekiti wa maisha.......PESA MBELE, mengine baadaye.....tehetehetehe amakweli 'WASIO-NA-HAYA-WANA-CHAMA-CHAO'!!!! hahahah

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad