Chama cha Wanasheria Tanzania Watoa Tamko Kuhusu Shambulizi Juu ya Mbunge Tundu Lissu

Sisi Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tangangika (Tanganyika Law Society, TLS) tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa tukio la Rais wa chama chetu, Mh. Tundu Lissu, kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake huko Dodoma leo hii mchana. Taarifa tulizo nazo mpaka sasa ni kwamba Mh Tundu Lissu bado yupo hospitali kuu ya Dodoma akipatiwa matibabu ya dharura. Tunamuomba Mungu azidi kumlininda na kumhifadhi Mh Tundu Lissu.

Kwa vyovyote vile, hivi sasa bado ni mapema sana kujua ni nani hasa wahusika wa tukio hili la kinyama na dhamiri yao, lakini, kwa niaba yetu na wanachama wetu, mawakili wa Tanganyika, tunalaani na kukemea vikali kitendo hiki cha kihalifu na cha uoga mkubwa.

Wito wetu kwa vyombo vya ulinzi na usalama ni kwamba wafanye kazi yao kwa umakini, haki na weledi ili kuwapata watu waliofanya unyama huu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake. Sisi kwa upande wetu tunalifuatilia suala hili kwa ukaribu, na tutaendelea kuufahamisha umma kinachoendelea.

Mwisho, tunatoa pole kwa familia ya Mh. Tundu Lissu, ndugu na jamaa zake, wanachama wetu wa Chama cha Mawakili Tanganyika na watanzania wote ambao wameguswa na tukio hilo. Tunaomba kila mmoja wetu kwa imani yake amuombee ndugu yetu Mh Tundu Lissu apone na apate nafuu haraka ili tuungane naye tena katika shughuli zetu za kila siku.
Tunawaomba wanachama na watanzania wote waendelee kuwa wavumilivu na watulivu wakati huu. Na kuujumla wetu tulaani na kukemea kitendo hiki ambacho hakikubaliki katika mila na desturi zetu kama Taifa.
Ahsanteni.

Imetolewa na
Godwin Simba Ngwilimi (Wakili), Makamu wa Rais, TLS,
Kwa niaba ya Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Poleni TLS..japo huyu kwenu ni mgeni kiutendaji .... Je alipata kuwaelezea kinachoendelea kuhusu matatizo yako yanayoendelea au mliwahi kumdadisi juu ya take over.

    CDM ni Si yamchezo....!!! inafikia hadi ya kutaka kumpa kilema mwanachama mwenzao .
    Kisa.... Anampiku Mwenyekiti wake...
    Mtajieleza toka HAI mpaka Nyiramba.
    Mlijaribu kwa Maskini Jito akaenda kkukiki huko akti. Sasa huyu bado hajaanzisha chama kipya
    mnataka funga kazi. Haya Dlama ndiyo inaanza.
    Kwani mtigwa amesema nini huko Kihesa??
    Hisia zipo na Dalili ni Dhahiri.
    Cdedma mtatueleza!!!!! na Ben sanane pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad