Changamoto ya Ajira Na Hatua Za Kuchukua Kwa Wahitimu Ambao Bado Hawajapata Ajira

Katika kipindi cha leo nakwenda kukushirikisha kuhusu changamoto ya ajira na hatua za kuchukua kwa wahitimu ambao hawajapata ajira.

Hili liko wazi sasa ya kwamba ajira ni changamoto. Mara zote tunaona nafasi chache za kazi zinazotangazwa, wanaomba watu wengi mno. Wahitimu ni wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana.

Hali hii imekuwa inawaumiza vijana wengi ambao wameishi maisha yao yote wakiambiwa wasome kwa bidii, wafaulu na watapata ajira nzuri na kuwa na maisha mazuri.

Vijana wanakazana kusoma kweli, wanafaulu na kuhitimu, lakini ajira zinakuwa changamoto.

Katika kipindi cha leo nimezungumzia mambo matatu muhimu sana;
1. Jambo la kwanza ni kuendelea kuomba kazi kwa wale ambao ndiyo wamehitimu, lakini wakati huo wasiruhusu maisha yao kusimama wakisubiri ajira. Badala yake waendelee kufanya mambo mengine pia.

2. Jambo la pili ni kufanya maamuzi magumu ya kuachana na harakati za jira, hasa pale ambapo umehitimu zaidi ya miaka miwili na umetafuta ajira bila ya mafanikio.

3. Jambo la tatu ni hatua za kuchukua, hapa nimekushirikisha ufanye nini sasa pale ambapo umefanya maamuzi magumu ya kuachana na zoezi la kutafuta ajira na kushika hatamu ya maisha yako. Nimekushirikisha maeneo ambayo unaweza kuanzia na ukaweza kupiga hatua kwenye maisha yako.

Download Application ya Ajira Yako Inayoweka Nafasi za Ajira Mpya Kila Asubuhi HAPA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad