CRDB Yampa PAUL Makonda Milioni 100 Kusaidia Ujenzi wa ofisi za Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari

CRDB Yampa PAUL Makonda Milioni 100 Kusaidia Ujenzi wa ofisi za Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari
Paul Makonda
Benki ya CRDB leo Jumatatu imekabidhi msaada wa Sh100 milioni kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule za msingi na sekondari mkoani hapa.

Mbali na kukabidhi fedha hizo, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, DK Charles Kimei ameahidi kuongeza Sh100 milioni katika bajeti ijayo.

"Mwalimu ndio chanzo cha maarifa ya kila mtu, tukitengeneza mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwake hata elimu inayotolewa itakua na kiwango," amesema Dk Kimei.

Amesema ili Taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo ni lazima kuwekeza katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na kuweka mazingira bora ya ufundishaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ya Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Charles Mbuge alimhakikishia Dk Kimei kuwa pesa zilizotolewa zitafanya kazi iliyokusudiwa.

"Thamani ya pesa iliyotolewa italingana na kile kitakachofanyika na hii iwe chachu kwa benki nyingine kuweza kuchangia ujenzi huu," amesema Kanali Mbuge.

Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya shule 638 zikiwa na upungufu wa ofisi 402 za walimu.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Paul Makonda, au Bashite sijui ni nani kati ya hawa wawili ni mcha Mungu, msemakweli. Na simjui kati ya hawa wawili ni kinyonga. Kinachonishangaza, Kati ya Wakuu wa mikoa yote ya Tanzania, Ni Paul makonda tu anayepata misaada kutoka mashirika, makampuni na Wachina . Zidi ya mkuu wa mkoa yeyote. Kuna kitu kimejifificha nyuma ya huyu Bashite Paul kikubwa sana na kwa hali ya juu inabidi asifiwe kila siku wakifikiri Watanzania watasau ni nani huyu kijana, na nini amekifanya hadharani, na kinaphitaji kupakwa mafuta matakatifu juu ya uozo fulani. Kitanuka tu,. Msijidanganye.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad