Dawa za Asili zinazoondoa Maumivu Wakati wa Hedhi Kwa Mwanamke

Wanawake wote hutokewa na kupata na hedhi mara moja kila mwezi na ni jambo la kawaida kwao kama wanawake. Hata hivyo wengi wao hupatwa na matatizo siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo haya hutofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine kutegemeana na afya ya muhusika.

DALILI ZA TATIZO HILI NI KAMA ZIFUATAZO:

Siku chache kabla ya hedhi, mhusika hupatwa na:

1. Kichwa kuuma
2. Msongo wa mawazo (stress)
3. Hofu na hasira za hapa na hapa
4. kuvimba sehemu za siri
5. Kukosa usingizi na
6. Matiti kujaa

Hali hii hutokea kwa sehemu kubwa kama matokeo ya homoni kutokuwa kuwa sawa (Homone imbalance) na hali hii inaweza kukoma ndani ya siku 1 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Dawa zinazoondoa maumivu wakati wa hedhi

1. JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO

Tumia juisi ya mchanganyiko huu: Kotimiri (Parsley), viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja kutwa mara 2.

2. TANGAWIZI

Tangawizi ni moja ya dawa nzuri sana ya asili linapokuja suala la kutibu na kutuliza maumivu wakati wa hedhi. Tengeneza chai ya tangawizi na unywe kikombe kimoja (robo lita/ml 250) kutwa mara mbili mara baada ya chakula cha mchana na baada ya chakula cha usiku. Unaweza kuweka mazoea ya kunywa dawa hii kila siku 3 kabla ya kuanza siku zako na ukaendelea hivyo wakati wote unapokuwa kwenye siku, na unashauriwa kuishi hivi kila mara ili kujijengea kinga mwili wako dhidi ya tatizo hili.

3. UFUTA

Dawa nyingine inayotibu tatizo hili ya asili isiyo na madhara yoyote kwa mtumiaji ni UFUTA. Dawa hii pia ni nzuri kwa wale wenye tatizo hedhi kidogo.

Hata hivyo kwenye majaribio kadhaa ufuta umeonekana kufanya kazi vizuri zaidi kwa wasichana wadogo kuliko kwa wamama watu wazima.

Namna ya kutumia: Saga ufuta kiasi upendacho na utumie kijiko kikubwa kimoja cha chakula ndani ya kikombe kimoja (robo lita au ml 250) kutwa mara 2.

Ufuta pia unaweza kupondwapondwa kiasi cha kiganja cha mkono wako na kuchanganywa katika maji yako ya kuoga ya uvuguvugu na utapata nafuu kubwa pia dhidi ya maumivu haya hasa ukianza kutumia siku 3 kabla ya kuanza siku.

4. PAPAI

Tuna kila sababu ya kusema ahsante kwa Mungu kwa kutukirimia mimea na miti mingi ambayo ni dawa kwa maradhi mengi yanayotusumbuwa.

Papai ni moja ya dawa za asili zinazoondoa maumivu wakati wa hedhi na linatajwa na watafiti mbalimbali kuwa ni msaada mkubwa kwa wasichana wanaopatwa na tatizo la kutokuona kabisa siku zao kama matokeo ya stress au mifadhaiko mingi ya kimaisha.

Ili liwe dawa unashauriwa kula kila mara tunda hili hasa lile ambalo halijaiva sana lakini tayari limekoaa na hata ile rangi ya ukijani iwe haijaondoka yote. Hii iwe ni tabia yako kusishi hivi kama una tatizo hili la maumivu wakati wa siku zako au hupati kabisa kuona siku.

Papai huweza haya yote kutokana na sifa yake kuu ya kuweza kulainisha misuli katika njia ya uzazi na hatimaye kuwezesha utokaji wa hedhi kuwa mrahisi bila maumivu yoyote. Jaribu hili na uniletee majibu.

5. MSHUBIRI (Aloe vera)

Hii ni dawa nyingine ya maajbu ya asili ambayo inatibu maradhi mengi mengi sana mwilini bila idadi ikiwemo hili la kupunguza au kuondoa kabisa maumivu wakati wa hedhi.

Matumizi: Changanya jeli ya Aloe vera (maji maji ya mshubiri) na pilipili manga nyeusi ya unga kidooogo, meza kijiko cha chakula kimoja mara tatu kwa siku kila siku hadi maumivu yatakapoacha.

6. NDIZI

Utashangaa sana kuona kumbe hata ndizi ni dawa na ingekuondolea maumivu hayo bila gharama yoyote. Wataalamu wamethibitisha pasipo na shaka kuwa ndizi mbivu zinao uwezo wa kutibu tatizo hili.

Nguvu ya ndizi kutibu hili zinatokana na ukweli kwamba ndizi ina B6 na madini ya chuma vitu viwili vinavyoweza kusaidia kurekebisha kiwango cha sukari, kuondoa au kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya kupooza, kuweka sawa shinikizo la damu na kudhibiti tatizo la upungufu wa damu kama matokeo ya siku zako.

Matumizi: Kula ndizi mbivu mbili mpaka tatu siku 4 kabla ya kuanza siku zako na wakati wote unapoendelea na siku zako. Kwa kifupi jizoeshe kuongeza tunda hili kwenye kila mlo ikiwa wewe ni mhanga wa tatizo hili la maumivu wakati wa hedhi na hutachelewa kuanza kuona tofauti. Kumbuka pia kutumia chumvi ya kutosha (hasa ya mawe kwenye vyakula vyako) kama unakula ndizi mara kwa mara ili kuiweka sawa potasiamu iliyomo kwenye ndizi ambayo nayo ikizidi huleta tatizo la kukakamaa kwa mishipa mwilini.

7. MAJI YA KUNYWA

Hii ndiyo dawa namba 1 na mhimu zaidi kuliko zote na ni ya lazima itumike na yeyote. Sababu kuu ya maumivu haya kama nilivyoyapeleza mimi ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha na hii ni matokeo ya watu kusubiri ndipo wanywe maji jambo ambalo ni kosa kubwa tunalifanya dhidi ya miili yetu bila kujuwa. Kila siku iendayo kwa Mungu kunywa maji lita 2 mpaka lita 3, kunywa kidogo kidogo kutwa nzima, maji ya kawaida siyo ya kwenye friji na hutakaa uone maumivu katika siku zako. Mke wangu hajawahi kusikia maumivu haya sababu nyumbani kwangu suala la kunywa maji linajulikana tangu siku ya kwanza.

8. MDALASINI

Tengeneza chai ukitumia unga wa mdalasini, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 2 wakati wote wa siku zako au anza siku 2 kabla pia unaweza kuweka mazoea ya kuwa hiyo ndiyo chai yako kila mara ili iwe kama kinga. Kumbuka kutumia asali badala ya sukari kwenye hii chai

9. JUISI YA KAROTI

Kunywa juisi ya karoti fresh glasi 1 kutwa mara 2 wakati wote wa siku zako, unaweza pia kujenga mazoea ya kula karoti tu moja hadi mbili kila siku kujenga kinga dhidi ya ugonjwa huu. Juisi itakuwa rahisi kwa wale wa mjini na ambao wana blenda pia, kijijini kula karoti fresh kila siku.

10. MCHAICHAI

Kama unasumbuliwa na tatizo hili kila mara basi hamia kunywa chai ya mchaichai kikombe kimoja kutwa mara 2 kila siku huku ukitumia asali badala ya sukari. Kama unaweza tengeneza juisi ya mchaichai na unywe kikombe kimoja kutwa mara 2 pia wakati wote wa siku zako.

Dawa ni hizo na hakuna sababu ya kuendelea kuteseka na maumivu haya bila sababu. Utaniuliza nitumie kwa muda gani? hivyo ni vyakula tu unaweza kutumia mpaka utakapopona na unaweza kuendelea kuzitumia hata kama huumwi chochote. Unaweza kutumia moja tu au ukachagua mbili hadi 3 ukatumia kwa pamoja ila kumbuka dawa namba 7 ni lazima.

MAMBO YA MHIMU KUZINGATIA KILA SIKU:

1. Kula matunda na mboga majani kwa wingi kila siku, matango, matikiti maji nk

2. Jishughulishe na mazoezi madogo madogo ya viungo

3. Oga maji ya moto (kama unasumbuliwa na hili tatizo kila mara)

4. Tumia mafuta ya samaki kila mara kwenye vyakula vyako au unaweza kunywa tu yenyewe kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku

5. Pata muda wa kutosha wa kulala usingizi masaa 7 mpaka 8 kila siku

6. Acha kula nyama nyekundu, sukari (tumia asali badala yake), usitumie unga wa ngano mweupe (uliokobolewa), usitumie sembe (kula dona).

7. Achana na msongo wa mawazo (stress)

8. Usivae nguo za kubana sana wakati wa siku zako

9. Acha chai ya rangi, kahawa, vilevi vyote, soda na vinywaji baridi vingine vyote (hii ni kwa mgonjwa usinielewe vibaya, kama huumwi chochote vitumie isipokuwa vilevi havifai kwa yoyote uwe unaumwa au huumwi).

Source:FadhiliPaulo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad